Siku ya Watoto Waadventista Duniani 2023

General Conference

Siku ya Watoto Waadventista Duniani 2023

Fursa kwa watoto ulimwenguni pote kuwa mawakala wa upendo na wanafunzi wa “Nitaenda!”

Inasemekana kila mara kuwa Watoto ni kanisa la Kesho. Tukiwa na takriban Watoto Zaidi ya milioni mbili wakiwa chini ya miaka 15 wanaoshiriki kanisa za kiadventista katika mwaka wa 2021, kukua na kuimarika kwa Watoto hawa, bila shaka huadhiri kesho ya kanisa la Kiadventista. Hata katika umri mdogo, yesu huita Watoto wawe mawakala wa pendo lake kwa ulimwengu.

Kanisa la waadventista linatazamia kusherehea siku ya Vijana ulimwenguni mnamo machi 18, 2023. Katika sherehe hii ya mwaka ambayo hufanywa kila sabato ya tatu ya machi, “Maelfu ya Watoto kutoka kote duniani watajiingiza na matendo ya kusaidia katika jamii zao, Alisema Dr. Orathai Chureson, Mkuu wa idara ya Watoto ulimwenguni. Mada ya mwaka huu ni “ Upendo ni kitendo”

Sherehe hii ya kila mwaka ni nafasi ya kutambua umuhimu wa Watoto na sehemu wanaichukua katika kanisa, katika misheni ya kristo na ulimwengu mzima.

Churen aliongeza, Siku hii huwapa Watoto nafasi kujiingiza katika vitendo vya kuonyesha huduma yao ya huruma, kusambaza upendo wa mungu kwa Rafiki zao na jirani na kuchangia kueneza injili ya milele.

Mawakala wa Upendo

Upendo wa kujitolea ni mada kuu kote kwenye maandiko ( 1 yohana 4:8) Chureson aliongeza, “ Upendo ni kuhusu kitendo.” Ingawa Watoto huwa wanamtazamo binafsi, aliongeza. Ni kwa jinsi hio alisisitiza umuhimu wa kuwafunza kuhusu upendo wa mungu na kuwapa nafasi nyingi kuuonyesha upendo kwa wengine

Watoto, jinsi ya wanafunzi wa yesu na wakristo wanafaa kufunzwa fikira za mkristo, wafunzwa upendo wa mungu na kujifunza kupenda kwa kujitolea, hata ingawa njia zao finyu za kuwa mawakala na kazi kwa kujitolea kwa wengine , iwe kanisa au katika jamii ili wakakuwe kwa kimo vile vile kwa roho wa kweli, alisema

Chureson anasemaje, Hizi tabia za kupendeza inafaa kupewa nafasi ili kukuwa, kukaza na kuhakikisha kuwajibika na kuhakikisha mawaza mazuri kuonyesha jambo la busara na la kumpendeza mungu

Kwa hivyo, kanisa la Adventista inahamasisa washiriki kusherehekea siku ya vijana ulimwenguni kwa kutambua hitaji la watu wa jamii na kuwajumuisha Watoto kusaidia kwa njia ya pekee. Kwa mfanno, kusaidia nguo kwa wale wanamahitaji au kuwa kufanya kazi ni baadhi ya mifano ya program za kanisa kulingana na mzingira

Tangu sherehe hii huambata na sherehe ya kiadventista ulimwenguni. Churesoni anaongeza kuwa kanisa nyingi husaidiia wanarika kujiunga na kazi.

Jinsi ya Kusherehekea Siku ya Vjiana ulimwenguni

Kama kanisa la waadventista ulimwenguni wanapojiandaa kwa sherehe hii, Viongozi wa kanisa ulimwenguni wameandaaa kusanyiko la mafundisho Adventist Global Children’s Day 2023An opportunity for children worldwide to be agents of love and disciples of “I Will Go!” ili kusaidia kanisa na viongozi kupanga sherehe ya kipekee na kuwajumuisha vijana katika programu.

Nyenzo ya Idara ya Watoto Waadventista Ulimwenguni 2023. [Picha: Imetolewa na Idara ya Huduma za Watoto ya Mkutano Mkuu.]
Nyenzo ya Idara ya Watoto Waadventista Ulimwenguni 2023. [Picha: Imetolewa na Idara ya Huduma za Watoto ya Mkutano Mkuu.]

Programu inajumuisha kukariri vifungu vya Bibilia kwa Watoto kusoma kila siku ya juma, maongezi, shughuli zinazotolewa kwa watu wazima kugawa na kuwafikia Watoto na mahubiri yatakayoweza kuigizwa kuwatia moyo Watoto kufanya huduma

Kwa miaka ya hapo awali, kusanyiko nyingi kote ulimwenguni wameandaaa huduma muhimu za Watoto kujiunga kwazo. Chureson akieleza kuwa Watoto ulimwenguni wamezuru familia za mayatima na familia zilizo na mahitaji ya kipekee wakati wa siku hii ya vijana ulimwenguni wakitoa zawadi na vitu muhimu kwa Watoto waliowakuta. Ilhali wengine waliwazuru wazee katika jamii zao, kuwafanya marafiki na kujitolea kuwasaidia na kazi za nyumbani.

Chureson anaongeza kuwa waadventista Watoto husafisha kanisa zao na kuokota uchafu kwa jamii zao na kanisa nyingi zimeripoti kukusanya na kugawa nguo kupitia kwa mpangilio wa nguo

“Watoto wamejitolea na akiba ya fedha zao kununua vitu muhimu na chakula kwa wengine walio na mahitaji, anasema Chureson.

Kutoka kwa program ya shule ya sabato hadi mahubiri, Chureson anasema inazingatia siku hii ya vijana ikizungumzia “huduma isiyo na ubinafsi” kwa wale walioko katika jamii zao.

Kama vile kanisa la waadventista wanapoongeza juhudi kila kona ya dunia yetu inayobadilika kila wakati na injili, yesu anaalika wanakanisa wachanga kushirikishwa katika misheni. Wacha tuwahimize na kuwapa nguvu Watoto waeneze, “Nitaenda” na wawe wanafunzi wa yesu kwa siku hii ya Watoto na kwa siku zote za mwaka.