Viongozi Akina Mama wa ADRA Wanahamasisha Ushirikishwaji kupitia Hadithi za Maisha

Adventist Development and Relief Agency

Viongozi Akina Mama wa ADRA Wanahamasisha Ushirikishwaji kupitia Hadithi za Maisha

Shirika linaadhimisha Mwezi wa Historia ya Akina Mama na Siku ya Kimataifa ya Akina Mama

Shirika la Maendeleo na Misaada la Waadventista (ADRA) liliheshimu Siku ya Kimataifa ya Akina Mama mnamo Machi 8 na Mwezi wa Kitaifa wa Historia ya Akina Mama kwa kuangazia hadithi za kushangaza za viongozi wa kike wa shirika hilo. Umoja wa Mataifa uliteua kaulimbiu ya 2024 ya Akina Mama kuwa mwaka wa kuhamasisha ushirikishwaji na kuwekeza katika maendeleo ya wanawake.

Kwa zaidi ya miaka 40, wanawake wa ADRA wametoa mchango mkubwa kwa jumuiya za kimataifa kwa kuhimiza ushirikishwaji na uwezeshaji kupitia mipango inayozingatia elimu, huduma za afya, na maendeleo ya kiuchumi. ADRA imekuwa na jukumu muhimu katika kutoa fursa na kukuza ushiriki kwa wanawake katika jamii ambazo hazijahudumiwa.

"Tunajivunia kusherehekea mafanikio ya ajabu ya viongozi wetu wanawake. Hadithi zao hutukumbusha uwezo na nguvu isiyo ya kawaida ambayo akina mama wanayo. Kwa kukuza ujumuishaji na kutoa fursa sawa, tunaweza kuunda ulimwengu wenye haki na ufanisi zaidi kwa kila mtu,” alisema Sonya Funna Evelyn[GT1] , makamu wa rais wa ADRA Kitaifa wa maendeleo endelevu.

Akina mama walioangaziwa katika toleo hili wanaonyesha mtandao dhabiti wa wahudumu wa kibinadamu ambao michango yao inaendeleza dhamira ya kimataifa ya ADRA ya kuharakisha maendeleo.

Maja Ahac, Mkuu wa Utetezi wa ADRA Ulaya

Maja Ahac anajitolea maisha yake kuwatetea wale walioondolewa sauti zao—mkimbizi, mtoto, mwanamke. Anasukumwa katika kazi yake na shauku ya kuhimiza wanawake wa rika zote kudumu katika ndoto zao.

Ingawa Ahaki anatumia siku zake kuwatetea akina mama bila woga, jukumu lake kama mama ndilo linalotia moyo kazi yake.

"Mimi ni mfanyakazi wa ADRA, lakini pia ni mama. Mimi ni mama wa msichana mmoja na wavulana wawili. Ni muhimu kwangu kwamba watoto wangu wote wawe na fursa sawa. Na hili ndilo ninalotaka kwa watoto wengine wote na wanawake wengine wote. Hatuwezi kufafanuliwa kwa jinsia na kuambiwa ‘hivi ndivyo unavyoweza kufanya’ au ‘hivi ndivyo uwezi fanya.’”

Ahac amekutana na mamia ya wanawake kutoka kote ulimwenguni kote katika kazi yake na ADRA. Anakumbuka vizuri uzoefu wake na mama anayeitwa Elisabeth wakati wa sherehe mpya ya shule nchini Burundi, Afrika Mashariki. Wakati watu wengine wa kijiji walisherehekea shule yao, Elisabeth alisimama akitazama kando, akimnyonyesha mtoto wake.

Ahac alimwendea Elisabeth na kumuuliza anafikiria nini kuhusu shule hiyo mpya. Akipuuza swali hilo, Elisabeth badala yake alimtazama Ahaki na kusema, “Ni vizuri sana kwamba umetutembelea. Mwanamke. Ulionyesha wasichana wetu kwamba wanawake wanaweza pia kusimamia miradi. Mashirika yanayoongoza. Kuwa wasimamizi na viongozi."

Ahac, pamoja na wafadhili wengine wengi wa kibinadamu wanaohudumu na ADRA, wanawatia moyo akina mama kila siku kwa kazi yao. Hata hivyo, ukimuuliza, atakuambia kwamba anachochewa zaidi na wanawake kama Elisabeth ambao waligusa maisha yake.

Sonya Funna Evelyn, Makamu wa Rais wa Kimataifa wa ADRA kwa Maendeleo Endelevu

Sonya Funna Evelyn ni jasiri na mwenye kujitolea, na kwa miaka 16 amekuwa akiwatia moyo akina mama anaowafikia kupitia kazi yake na ADRA, na wale wanaofanya kazi ndani ya mtandao wa ADRA.

Akiwa mzaliwa wa Sierra Leone, Afrika Magharibi, Evelyn alikuza hamu kubwa ya kusaidia wengine akiwa mdogo. Kuhamia Marekani akiwa mtoto kulimpa fursa ya kupata elimu na fursa ambazo familia yake ya nyumbani haikuwa nazo. Kuona jinsi familia yake huko Afrika Magharibi pia ililazimika kushughulika na changamoto za ziada kuanzia njaa hadi vurugu kulimtia moyo Evelyn kutafuta taaluma ya huduma za kibinadamu na kufanyia ADRA kazi.

“Somo muhimu zaidi ambalo nimejifunza katika kazi hii ni kwamba ulimwenguni pote watu wako sawa. Sisi sote tunataka vitu sawa kutoka kwa maisha. Tofauti pekee ni katika uwezo wetu wa kupata vitu hivyo,” anasema.

Evelyn ameshuhudia ukuaji mkubwa na mabadiliko ndani ya ADRA katika kipindi chake cha utumishi. Katika yote hayo, akina mama wamekuwa katikakati.

"Akina mama wanaofanya kazi katika ADRA ni maalum kwa sababu wamejiandikisha kukabiliana na changamoto kubwa. Na bila wao, bila sisi, shirika hili lisingekuwa kama lilivyo. Na kwa hivyo, hatuwezi kuzungumzia ni wapi ADRA inakwenda katika siku zijazo ikiwa hatuzungumzii pia uongozi wa kike.”

Evelyn ni sehemu muhimu ya uongozi wa ADRA. Alijiunga na shirika kama mshauri wa kiufundi wa afya na sasa, kama makamu wa rais, anatoa uongozi wa kimkakati kwa ukuaji wa siku zijazo kwani ADRA inatekeleza mfumo mpya wa kimkakati wa kimataifa.

Anapoelezea mabadiliko ya ADRA katika miongo kadhaa iliyopita, Evelyn anasema, "Sio jambo linalotokea kwa bahati mbaya. Ni kwa sababu nguvu za akina mama kwa pamoja zinaweza kufikia mambo yasiyopimika. Na ukiangalia hata kazi tunayofanya kwenye uwanja huo, data inaonyesha kwamba ikiwa unataka kuleta mabadiliko katika jamii, toa fedha kwa akian mama. Kwa sababu akina mama watatengeneza upya nyumba zao, wamejitolea kwa kaya zao, wamejitolea kwa watoto wao. Na wana nguvu ya kubadilisha jamii nzima."

Leiza Augsburger, Mkurugenzi wa Mipango katika ADRA Uswisi

Leiza Augsburger alisomea sheria, lakini hata baada ya kuhitimu, aligundua kuwa haikuwa kazi aliyoitaka kufanya kwa sababu shauku yake ya kweli ilikuwa kufanya kazi na kuwa karibu na watu. Hapo ndipo Augsburger alipogundua ADRA kwa mara ya kwanza, na hajawahi kuangalia nyuma.

Augsburger amehudumu katika majukumu kadhaa na ADRA, ikiwa ni pamoja na mkurugenzi wa nchi wa ADRA Togo. Anapata msukumo katika kufanya wengine, hasa wanawake, wahisi kama wanathaminiwa na kutambuliwa. Augsburger anapenda kusimulia jinsi alivyokutana na kikundi cha akina mama ambao walihudhuria programu ya elimu ya msingi ya ADRA nchini Togo.

"Nilikutana na baadhi ya akina mama kutoka programu moja nchini Togo, mpango wa kusoma na kuandika, na walifurahi sana kunionyesha kwamba waliweza kutumia simu zao za rununu na kuweka nambari yangu katika simu zao za rununu peke yao," Augsburger anakumbuka.

Bila shaka, kila mtu katika Afrika ana simu ya mkononi na anajua jinsi ya kuitumia. Lakini akina mam hawa hawakuweza kusoma na hawakuwahi kutumia simu zao kwa kujitegemea.

Ingawa kwa wengi hili linaweza kuonekana kama jambo dogo, Augsburger anatambua kwamba hakuna kitu kinachotoa hadhi kwa mtu ni kidogo.

"Ninaamini kuwa mojawapo ya athari zenye nguvu zaidi za ADRA ni kwamba kazi yetu inawapa watu fursa ya kuwepo," Augsburger anasema. "Ona, wakati mwingine wanufaika wanahisi kama wako wazi. Hakuna anayewaona. Na kisha ADRA inaingia, labda na mradi mdogo ambao hauonekani wa maana sana kwetu, lakini tulichofanya ni kutambua kwamba watu tuliowahudumia ni wanadamu. Na tunawapa fursa ya kukua."

Judith Musvosvi, Mkurugenzi wa Nchi wa ADRA Zimbabwe

Judith Musvosvi amejitolea kwa misheni ya kutoa misaada ya kibinadamu kwa zaidi ya muongo mmoja. Alijiunga na ADRA mwaka 2013 kama mkurugenzi wa nchi wa Zimbabwe. Katika muda wake katika ADRA, amesimamia mamia ya miradi na kuelekeza juhudi nyingi za kukabiliana na dharura. Kinachomtia moyo zaidi ni jinsi mtandao wa ADRA huja pamoja mara kwa mara ili kuleta mwanga katika hali mbaya zaidi.

Alipoulizwa kuhusu uzoefu wake wa kufanya kazi na mtandao wa ADRA, Musvosvi mara kwa mara anataja familia yake ya Waadventista. Shirika linajivunia kuwa mshiriki wa mtandao wa kimataifa unaojumuisha maelfu ya makutaniko ya Waadventista Wasabato ambayo huungana haraka wakati wa matatizo.

"Kinachotenganisha ADRA ni kile tunachoweza kufikia kama mtandao na familia," Musvosvi anasema. "Hiyo inashinda chochote ambacho tutaweza kutimiza kama watu binafsi."

Musvosvi ameshuhudia ujasiri wa familia ya ADRA wakati wa kukabiliana na changamoto katika nchi yake. Timu yake mara nyingi huwa ya kwanza kujibu na kutoa msaada, shukrani kwa ushirikiano mkubwa na makanisa ya mitaa ya Waadventista na mashirika mengine yasiyo ya kifaida.

“Kile ningependa watu wafahamu kuhusu ADRA ni kwamba sisi tunaofanya kazi na ADRA tuna dhamira ya kweli kuhusu kazi tunayofainya. Jambo linalotuzunguka ni lile la kuwajali kweli watu," asema Musvosvi.

ADRA inatumai kuwa kushiriki uzoefu wa viongozi wa kike ndani ya mtandao wake wa kimataifa kutakuza utambuzi na kuthamini mafanikio ya akina mama duniani kote.

This article was provided by ADRA International.