General Conference

Makamu wa Rais wa Mkutano Mkuu Maurice R. Valentine II Apumuzika

Valentine atakumbukwa kama kiongozi mwenye maono katika mawasiliano ya kidijitali na vyombo vya habari na kiongozi aliyesikiliza

United States

Mnamo Oktoba 20, 2023, Maurice R. Valentine II, mtumishi aliyejitolea wa Kanisa la Waadventista Wasabato amepumuzika. [Picha: Brent Hardinge/Adventist Media Exchange (CC BY 4.0)]

Mnamo Oktoba 20, 2023, Maurice R. Valentine II, mtumishi aliyejitolea wa Kanisa la Waadventista Wasabato amepumuzika. [Picha: Brent Hardinge/Adventist Media Exchange (CC BY 4.0)]

Mnamo Oktoba 20, 2023, Maurice R. Valentine II, mtumishi aliyejitolea wa Kanisa la Waadventista Wasabato, aliaga dunia, na kuacha urithi wa kujitolea kwa imani yake bila kuyumbayumba na kazi ya kuvutia ya uongozi ndani ya kanisa la Waadventista. Alikuwa na umri wa miaka 63.

Valentine alikuwa makamu mkuu wa rais wa Konferensi Kuu (GC) ya Waadventista Wasabato wakati wa kifo chake. Ted Wilson, rais wa GC alishiriki, “Kifo cha Mchungaji Maurice Valentine ni msiba kwa Kanisa la Ulimwengu. Alikuwa kiongozi mcha Mungu sana na sehemu muhimu ya timu yetu ya uongozi wa Kanisa la Ulimwengu. Mioyo yetu imevunjika kwa habari hizi za kusikitisha.”

Safari ya Valentine katika huduma ilianza mwaka wa 1985, akihudumu kama mchungaji katika makanisa mbalimbali kote Colorado, Iowa, Missouri, na Nebraska zaidi ya miaka 28. Maisha ya Valentine ya uongozi wa utumishi yalimpelekea kuwa mkurugenzi wa huduma wa Konferensi ya Unioni ya Amerika ya Kati kuanzia 2006 hadi 2012, na kuendeleza athari zake kwa kanisa. Baadaye aliitwa kwenye Konferensi ya Majimbo ya Kati, kama msaidizi wa rais, makamu wa rais wa utawala (katibu mtendaji), na rais.

G Alexander “Alex” Bryant, rais wa Divisheni ya Amerika Kaskazini, alitafakari kuhusu uhusiano wake na Valentine, akishiriki, “Mimi na Maurice tulijuana kwa zaidi ya miaka 40 kupitia maisha yetu ya chuo kikuu na huduma. Sikuzote Maurice alikuwa na shauku kwa Mungu, familia yake, na huduma.” Bryant na Valentine walihudhuria Chuo cha Oakwood (sasa Chuo Kikuu cha Oakwood) pamoja, ambapo wakawa marafiki. Baadaye, walipata fursa ya kuhudumu pamoja kama washirika katika utume katika Konferensi ya Majimboya Kati. Bryant alithibitisha uongozi wa Valentine akisema, "Alitekeleza wajibu wake kwa kiwango cha juu cha ubora na taaluma. Sikuzote angepata maneno ya kutia moyo ya kuongea na wale aliokutana nao na alichukua wakati kuwasikiliza, hasa katika nyakati za giza sana.”

Kenneth Denslow, rais wa Konferensi ya Unioni ya Lake alishiriki, “Maurice alitumikia Konferensi ya Unioni ya Lake kwa uaminifu kama katibu na kisha kama rais. Katika majukumu yoyote aliyotumikia, sikuzote alikuwa mwaminifu kwa Kristo, kanisa, na utume wake. Mioyo yetu inaumia kwa hasara hii. Maombi yetu yako kwa Sharon na familia."

Mnamo Aprili 2021, Valentine alihamia Divisheni ya Amerika Kaskazini (NAD) kuhudumu kama makamu wa rais kwa huduma za vyombo vya habari, ambapo aliendeleza utume wa Kanisa katika hali ya mabadiliko ya haraka ya mazingira ya vyombo vya habari. Richard Stephenson, mweka hazina msaidizi wa GC, alihudumu naye katika NAD na GC, na akamkumbuka kama mwotaji wa kweli wa media za kidijitali na uinjilisti mkondoni. Stephenson alieleza, “Nimekuwa na fursa kubwa ya kufanya kazi kwa karibu na Maurice na alikuwa mshauri wangu katika kutafuta njia mpya na bunifu za kuhubiri Yesu. Alishiriki nami mara nyingi imani yake kwamba Kanisa lazima litumie vyema vyombo vya habari na teknolojia ili kuungana na kushirikiana na wale wanaomtafuta Yesu. Mojawapo ya Kamati alizoongoza katika Konferensi Kuu ilikuwa Ubunifu wa Kidijitali ambao unatafuta kutumia teknolojia mpya na zinazoibukia kuendeleza Injili, inayolingana kikamilifu na uongozi wake wenye maono.” Akimwita Valentine jitu la kiroho, Stephenson aliendelea, “Zaidi ya haya yote, alimpenda Bwana wake, na shauku yake ilikuwa kwa Kanisa kutumia kila mbinu kuwaambia wengine kuhusu Yesu na uwezo Wake wa kubadilisha maisha. Jitu la kiroho la mtu limepumzika.”

Athari ya Maurice R. Valentine II ilienea zaidi ya vyeo vyake, kama alivyojulikana kwa upole, uadilifu, na ufahamu wake wa kina wa kimishenari. Kuchaguliwa kwake kama makamu wa rais wa GC katika Kikao cha GC cha 2022 kulikuwa ushahidi wa zawadi zake za kipekee. Audrey Andersson, ambaye pia alichaguliwa kuhudumu kama makamu wa rais katika kikao cha 2022, alitafakari, "Baada ya kuchaguliwa wakati huo huo, nilihisi uhusiano maalum na Maurice. Alikuwa jitu la imani. Daima ni mkarimu, mwenye adabu na mwenye kujali. Angepitia kwa ofisi yangu kwa mazungumzo na maombi. Hakuna mtu ambaye angeweza kukutana na Maurice na kutoguswa na mwenendo wake mchangamfu wa Kikristo. Kanisa limempoteza kiongozi wa ajabu. Familia yake imempoteza baba na mume wenye upendo. Sisi ambao tulikuwa na pendeleo la kufanya kazi naye tumepoteza rafiki na mfanyakazi mwenza wetu wa thamani.”

Tunapotafakari maisha ya huduma aliyoishi Valentine, tunatazamia siku ambayo tutamwona kwa mara nyingine tena. Ted Wilson, analihimiza kanisa la kimataifa “tafadhali mwombee kwa bidii mke wake, Sharon, na familia nzima ya Valentine.” Anaongeza, “Mioyo yetu inatiwa moyo na uhakika wenye kutia moyo kwamba Yesu anakuja hivi karibuni!”

Valentine ameacha mke wake mpendwa, Sharon (Livingston) Valentine, na watoto wao watatu wazima. Maisha yake na michango yake kwa Kanisa la Waadventista Wasabato itakumbukwa kwa heshima kubwa na shukrani.

Any comments left below will be sent to the family.