South Pacific Division

Wafanyakazi wa Shule ya Waadventista nchini Tonga Wapokea Biblia Maalum za Kuimarisha Imani na Maisha ya Kitaaluma

Mradi huu utahakikisha wafanyakazi wote katika Divisheni ya Pasifiki Kusini wanapokea Biblia ya Abide katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Mchungaji Glenn Townend akikabidhi mojawapo ya Biblia kwa Mwalimu Mkuu wa Chuo cha Waadventista cha Beulah, Lemani Matui.

Mchungaji Glenn Townend akikabidhi mojawapo ya Biblia kwa Mwalimu Mkuu wa Chuo cha Waadventista cha Beulah, Lemani Matui.

[Picha: Adventist Record]

Wafanyakazi katika shule za Waadventista nchini Tonga wamepokea Biblia mpya iliyoundwa maalum kwa ajili ya kukuza imani yao na kuunga mkono muda wao binafsi na Mungu.

Wakati wa ziara ya hivi karibuni huko Tonga, Glenn Townend,Rais wa Divisheni ya Pasifiki Kusini (SPD), alibeba nakala za Biblia ya Abide kwa ajili ya wafanyakazi wote wa shule. Alisema Biblia hizo hazikuwa tu kwa walimu, bali pia kwa wapishi, wakulima, madereva wa basi na wafanyakazi wengine.

“Biblia ni ya kuwakumbusha wakae ndani ya Kristo,” alisema, “kuwahimiza waishi maisha yao ya kiroho katika taaluma zao.”

Biblia ya Abide ina rasilimali za ziada zilizoundwa na kukusanywa na Murray Hunter, Katibu Msaidizi wa Huduma ya Ushauri (Ministerial Associate secretary for Chaplaincy) wa Konferensi ya Yunioni ya Australia , maalum kwa ajili ya kuunga mkono wale wanaofanya kazi katika elimu ya Waadventista Pasifiki Kusini.

Mradi huo, unaoungwa mkono na kufadhiliwa na SPD na yunioni zake nne, utaona wafanyakazi wote katika idara hiyo wakipokea Biblia ya Abide katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Makala asili yalichapishwa kwenye tovuti ya habari ya Divisheni ya Pasifiki Kusini, Adventist Record.