South American Division

Uchangiaji wa Damu Huimarisha Hisia ya Utume wa Vijana Waadventista nchini Brazili

Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, kampeni ilichangia zaidi ya mifuko milioni 1 na laki 2 ya damu iliyotolewa katika nchi nane za Amerika Kusini.

Wachangiaji damu mbele ya kituo cha damu cha Brasilia, katika mji mkuu wa shirikisho.

Wachangiaji damu mbele ya kituo cha damu cha Brasilia, katika mji mkuu wa shirikisho.

[Picha: Thiago Fernandes]

Amanda Santos Barbosa ni mfundi wa uuguzi anayeishi Maraú, Bahia nchini Brazil. Alikuja kushiriki katika Kongamano la Vijana la Maranatha, na alipojua kwamba moja ya matendo yake yangehusiana na mradi wa Vida por Vidas (Maisha kwa Ajili ya Maisha), aliamua kutoa mchango wake wa kwanza wa damu.

Profesa Rosan Dias de Aguiar anaishi katika mji wenye wakazi 4,000 kusini mwa jimbo hilo hilo. Katika kanisa la Waadventista analohudhuria, vijana wanashiriki katika mipango ya huduma. Ili kuchanga, wanapaswa kwenda kwenye jiji la karibu zaidi, Eunapolis, umbali wa saa tatu hivi. Lakini umbali sio kizuizi. "Kujua kwamba ulisaidia, kwamba mtu fulani alikuwa na maisha bora, au kwamba yalibadilishwa na damu uliyotoa ni jambo la kufurahisha sana," alisema.

Kama vile Barbosa na Dias, washiriki wengi kutoka kwenye kusanyiko walikuwa kwenye kituo cha huduma ya damu cha Brasilia ili kusaidia kuhakikisha kuwepo kwa mifuko kwenye akiba. Katika Wilaya ya Shirikisho la Brazili pekee, kitengo cha kukusanya huhudumia hospitali 19.

Mfuko mmoja wa damu unaweza kunufaisha watu hadi wanne.
Mfuko mmoja wa damu unaweza kunufaisha watu hadi wanne.

Kelly Barbi ni meneja wa eneo la kukusanya damu katika kituo cha huduma za damu cha Brasilia na alishukuru Kanisa la Waadventista Wasabato kwa ushirikiano wake wa muda mrefu kupitia mradi wa Life for Lives. “Mnao ufaafu mzuri sana, mtindo wa maisha wenye afya, na hilo linaturahisishia kazi, kwa sababu tunaweza kubadilisha wengi wa watu wanaokuja kwa mtazamo chanya kwa ajili ya mchango halisi,” alisisitiza.

Maisha kwa Ajili ya Maisha

Mwaka wa 2005, katika jimbo la Rio Grande do Sul, Life for Lives project (mradi wa Maisha kwa ajili ya Maisha) ulianzishwa kwa msingi wa mpango wa hiari ulioendelezwa na vijana Waadventista. Mradi huo ulipendekeza kuchangia vituo vya damu kupitia hamasa ya kutoa damu.

Mwaka 2006, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kuchangia Damu kwa Hiari Duniani huko Washington, Marekani, mpango huo ulitambuliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kama “Kampeni Bora ya Shirika la Afya la Pan American.” Mwaka huo huo, mradi huo ulianza kuwa sehemu ya kalenda ya shughuli rasmi za Kanisa la Waadventista katika nchi nane za Divisheni ya Amerika Kusini (SAD), mojawapo ya maeneo yanayohudumiwa na dhehebu hilo.

Vijana pia walitumia fursa hiyo kukuza mradi na mtindo wa maisha wa kujali na kuzingatia wengine.
Vijana pia walitumia fursa hiyo kukuza mradi na mtindo wa maisha wa kujali na kuzingatia wengine.

Katika miaka 10 iliyopita, kampeni imechangia zaidi ya mifuko milioni 1 na laki mbili ya damu iliyotolewa katika nchi nane za Amerika Kusini.

Makala asili ilichapishwa kwenye tovuti ya Kihispania ya Divisheni ya Amerika Kusini.