Mama Na Bintiye Wamurudia Yesu Baada Ya Miaka 16

Violeta akibatizwa katika Kongamano la Vijana la #ItsComing. (Picha: MNO)

South American Division

Mama Na Bintiye Wamurudia Yesu Baada Ya Miaka 16

Ingawa Irina aliamua kuacha kanisa, Mungu hakumwacha kamwe.

Irina na binti yake Celeste walishiriki katika shughuli za Kanisa la Waadventista katika mji wa Picota, ulioko katika msitu wa Peru. Hata hivyo, mume wa Irina hakukubali, hakuwaruhusu waende kanisani, na alifanya kila liwezekanalo ili kuwaweka mbali na imani.

Jinsi muda uliposonga, Binti mdogo wa Irina, Violeta, alijifungua. Hali ya familia ikawa ngumu. Shida zikazuka, na bwanake akaamua kutoka nyumbani, akimwacha peke yake na Watoto wake. Baada ya shida hizo katika Maisha yake, Irina aliacha ushirika wa kanisa, lakini aliitunza Imani yake kwa mungu.

Celeste na Violeta wakishiriki katika siku 10 za maombi. (Picha: Daniel Hanco)
Celeste na Violeta wakishiriki katika siku 10 za maombi. (Picha: Daniel Hanco)

Irina alijituma sana kufanya kazi ili aitunze familia. Ingawa, katika miaka ile, mungu alimlinda na akawahifadhi Watoto wake. Irina hakuwai kufikiria juu ya mwaliko wa mwanawe mdogo kujiunga na ushirika wa wanarika kungewafanya wakutane na familia yao, kanisa lao na mungu wao.

Violeta alibatizwa katika kongamano la vijana lililoitwa “it is coming” lililofanyika eneo la Universidad Peruana iliyo kule Lima, sabato ya tarehe 18, Februari 2023. Kutokana na uamuzi huu wa bintiye mdogo, Irina and Celeste waliamua kurudi kanisani baada ya miaka 16.

Mchungaji Daniel Hancco akiwa na Violeta, Irina na Celeste. (Picha: Daniel Hanco)
Mchungaji Daniel Hancco akiwa na Violeta, Irina na Celeste. (Picha: Daniel Hanco)

“Mungu kutoka mwanzo hakutuacha pweke. Alikuwa akishikilia hatamu ya Maisha yetu. Dada yangu mdogo alibatizwa, mwendani wangu atafunza Upeu Tarapoto, na naona mungu katika Maisha yangu kwa sababu ya ushindi alionipa. Inaoneka mungu anafanya vitu vyote sawa ili tukaweze kurudi kanisani,” Alisema Celeste, ambaye pamoja na mamake, walifanya uamuzi wa kupeana Maisha yao upya kwa yesu katika sabato ya machi 4, katika mkusanyiko wa injili wa Reencuentro.

The original version of this story was posted on the South American Division Spanish-language news site.