Tarehe 7 Juni, 2024, katika Shule ya Manispaa ya Emiki Kawamura Sakitani iliyopo Mato Grosso do Sul, Brazili, tukio la kishujaa lilitokea. Adrian Gonçalves mwenye umri wa miaka kumi na mbili aliokoa mwenzake aliyekuwa anakabwa koo wakati wa likizo.
Wakati wa tukio hilo, Gonçalves alikutana na rafiki yake akiwa matatani na, bila kusita, alitekeleza mbinu ya Heimlich. Alijifunza mbinu hiyo miezi mitatu iliyopita katika Klabu ya Pathfinder ya Buriti. “Nilipomwona rafiki yangu katika hali hiyo, sikusita kumsaidia, nikatumia mbinu nilizojifunza tulipokuwa tunafanya First Aid honor,” aliripoti kijana huyo mtafutaji.
Klabu ya Pathfinder ya Buriti, iliyoanzishwa mwaka 2022, iinajumuisha vijana 22 na hupokea msaada kutoka kwa baadhi ya wazazi kila siku. Kwa mujibu wa Gleice Minarini, mkurugenzi wa klabu hiyo, mafunzo hayo yalikuwa ya msingi. “Tulialika hospitali ya mji kuongoza pathfinders kuhusu huduma na msaada wa first aid. Kwa hakika, mmoja wa wataalamu waliofika kusaidia katika mafunzo haya alikuwa baba yake Adrian, ambaye ni muuguzi,” alieleza Minarini. Aliongeza pia kuwa, licha ya klabu hiyo kuwa na asilimia 100 ya washiriki wasio wa Kanisa la Waadventista, washiriki wote wanaonyesha ari kubwa ya mshikamano na kujifunza.
Mamake Adrian, Daiane Arruda, alionyesha kiburi chake kwa mwanawe. “Kama mama, ninahisi furaha sana kwa mtazamo wa mwanangu. Lakini pia najua jinsi ilivyo muhimu kwa watoto wetu kusaidiwa. Kuna sababu mbili za furaha yangu: moja kwamba mtoto aliokolewa na nyingine kwamba ni mwanangu ambaye alisaidia”, alisema Arruda. Pia aliangazia matokeo chanya ya Klabu ya Pathfinders katika maisha ya vijana. "Tuliona mabadiliko chanya katika tabia yake, kama vile ukomavu na uwajibikaji katika ahadi zake.''
Klabu ya Pathfinder inafundisha ujuzi muhimu wa maisha na kuandaa washiriki wake kujibu dharura mbalimbali. Gonçalves sasa anaonekana kama shujaa na wenzake na walimu wake, wamebainisha.
Makala asili ilichapishwa kwenye tovuti ya Kireno ya Divisheni ya Amerika Kusini.