South American Division

Kanisa la Waadventista nchini Argentina Linasheherekea Ukarabati wa Makao Makuu ya Konferensi ya Yunioni

Kituo hicho kipya kinanuia kuboresha huduma za kijamii na juhudi za uinjilisti kote nchini.

Argentina

Alexis Villar, Divisheni ya Amerika Kusini, na ANN
Ted Wilson anatoa ujumbe kwa wale waliopo katika makao makuu ya Konferensi ya Yunioni ya Argentina.

Ted Wilson anatoa ujumbe kwa wale waliopo katika makao makuu ya Konferensi ya Yunioni ya Argentina.

[Picha: Luis Sánchez]

Kanisa la Waadventista Wasabato nchini Argentina hivi karibuni liliadhimisha ufunguzi upya wa makao makuu ya utawala ya Konferensi ya Yunioni Argentina, yaliyoko katika eneo la kimkakati katika jiji la Vicente López, mkoa wa Buenos Aires.

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na Ted Wilson, rais wa makao makuu ya Konferensi Kuu ya Kanisa la Waadventista Wasabato, ambaye aliandamana na viongozi wa kitaifa wa kanisa la Waadventista.

Darío Caviglione, rais wa Kanisa la Waadventista nchini Argentina, alieleza furaha yake kwa ukarabati wa eneo hili, ambalo linatumika kama nyumba ya utawala na kituo cha uratibu kwa Kanisa kote nchini.

“Tulikuwa na furaha ya kupokea viongozi wetu katika makao makuu ya utawala ya Yunioni ya Argentina, ambayo ni nyumba ya Kanisa kwa nchi nzima na mahali ambapo maono ya utendaji wa Kanisa yanazalishwa na kusambazwa,” alisema.

Dario Caviglione anawasilisha ufunguzi upya wa makao makuu mapya ya Kanisa.
Dario Caviglione anawasilisha ufunguzi upya wa makao makuu mapya ya Kanisa.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi wa kidini kama vile Magdiel Pérez Schulz, msaidizi wa Rais katika GC; Stanley Arco, rais wa Divisheni ya Amerika Kusini; Edson Medeiros, mweka hazina wa SAD; na Bruno Raso, makamu wa rais wa SAD, miongoni mwa wengine.

Pia walikuwepo wasimamizi wa taasisi za Waadventista, kama vile Marcelo Cerdá, rais wa Alimentos Granix; Dkt. Haroldo Steger, mkurugenzi wa Sanatorio Adventista del Plata; Gabriel Cesano, rais wa Asociación Casa Editora Sudamericana; Dkt. Gustavo Weiss, mkurugenzi wa Clínica Adventista Belgrano; Horacio Rizzo, mkuu wa Chuo Kikuu cha River Plate; na Gabriel Boleas, mkuu wa Instituto Superior Adventista de Misiones.

Bwana Agustín Caulo, Naibu Katibu wa Ibada wa Taifa, akizungumza maneno ya shukrani kwa Kanisa
Bwana Agustín Caulo, Naibu Katibu wa Ibada wa Taifa, akizungumza maneno ya shukrani kwa Kanisa

Marais wa Mashirika na Misheni (ofisi za kikanda za Kanisa) zinazounda Yunioni ya Argentina pia walishiriki: Mchungaji Alejandro Brunelli, rais wa Shirika la Argentina ya Kati; Mchungaji Javier Holm, rais wa Shirika la Argentina ya Kaskazini; Mchungaji David Peralta, rais wa Shirika la Argentina ya Kusini; Mchungaji Elvio Silvero, rais wa Shirika la Buenos Aires; Mchungaji Marcos Zalgado, rais wa Misheni ya Argentina Magharibi ya Kati ; Mchungaji Iván Rosales, rais wa Misheni ya Argentina ya Kaskazini Magharibi; na Mchungaji Marcelo Coronel, rais wa Misheni ya Buenos Aires ya Kaskazini.

Mamlaka za kiraia pia zilihudhuria sherehe hiyo, ikiwa ni pamoja na Bwana Agustín Caulo, Naibu Katibu wa Ibada wa Taifa; Bi. María del Pilar Bosca Chillida, Mkurugenzi Mkuu wa Ibada wa Serikali ya Jiji la Buenos Aires; Bi. Soledad Martínez, Meya wa Vicente López; na Bi. Laura Caramella, Mratibu wa Ibada wa Manispaa ya Vicente López. Wakati huo huo, Jorge Macri, Meya wa zamani wa Vicente López, pia alieleza shukrani zake kwa jamii ya Waadventista kupitia ujumbe.

Soledad Martínez, Meya wa Vicente López, akisisitiza kazi ya pamoja na Kanisa katika mji huo.
Soledad Martínez, Meya wa Vicente López, akisisitiza kazi ya pamoja na Kanisa katika mji huo.

Jengo la awali lilikuwa limefunguliwa kwa zaidi ya miongo minne, lakini ukuaji wa Kanisa ulifanya iwe wazi kuwa lilihitaji usasaishaji na upanuzi.

“Tulihitaji sio tu kusasisha tulichokuwa nacho, bali pia kupanua ili kukidhi mahitaji mapya,” alieleza Caviglione. “Tunamshukuru Mungu kwa kutoa njia za kufanya hili liwezekane na pia kwa msaada wa Kanisa kwa ujumla, Divisheni ya Amerika Kusini na timu hiyo nzima.”

Wilson alisisitiza umuhimu wa jengo hili lililokarabatiwa kama chombo cha kuimarisha kazi ya Kanisa la Waadventista nchini Argentina.

“Jengo hili lazima liwe chombo cha kuhudumia Kanisa lote vizuri zaidi na, kwa hivyo, jamii. Tunamshukuru Mungu kwa kuruhusu upanuzi huu kuendelea na misheni yetu. Tunatumaini kuwa kila nafasi hapa itachangia huduma bora kwa watu na upanuzi wa ujumbe wa Waadventista,” alisema.

Ufunguzi wa mabamba kwenye mlango wa makao makuu ya Konferensi ya Yunioni ya Argentina.
Ufunguzi wa mabamba kwenye mlango wa makao makuu ya Konferensi ya Yunioni ya Argentina.

Eneo la jengo kwenye makutano ya barabara kuu mbili, Barabara Kuu ya Pan-Amerika na Barabara ya San Martin, linaifanya kuwa sehemu ya marejeo kwa jamii ya Waadventista na wale wanaopita eneo hilo.

"Ni mahali pa kuonekana ambalo kwa namna fulani liko katika moyo wa jamii ya Waadventista katika mtaa huu, lakini pia ni ushuhuda kwa wote wanaopita hapa," alisema Caviglione.

Zaidi ya umuhimu wake wa kimuundo, kiongozi wa Kanisa nchini Argentina alisisitiza kuwa umuhimu wa kweli wa makao makuu haya uko katika kusudi lake la kimisheni.

“Kuwa na jengo zuri, kubwa na la kisasa ni muhimu, lakini jambo muhimu zaidi ni kuweza kuzingatia misheni. Tunatumaini kuwa muundo huu unaweza kuwa njia ya kutimiza misheni kwa ufanisi zaidi,” alihitimisha.

Ukataji wa utepe kwenye mlango mkuu wa makao makuu. hayo.
Ukataji wa utepe kwenye mlango mkuu wa makao makuu. hayo.

Programu hiyo iliendelea jioni na matangazo maalum kwenye kituo cha YouTube cha Kanisa la Waadventista nchini Argentina, kilichoongozwa na Wilson. Kutoka kanisa la Florida, ambalo pia lilifunguliwa upya, alitoa ujumbe kwa nchi nzima. Wakati wa hotuba yake, alisisitiza umuhimu wa rasilimali mpya ambazo Kanisa linazo, daima kuwa njia ya kualika watu zaidi kumjua Yesu.

Wilson na mkewe Nancy, pamoja na binti yao Katherine na mjukuu Charlotte, wakikaribishwa Argentina.
Wilson na mkewe Nancy, pamoja na binti yao Katherine na mjukuu Charlotte, wakikaribishwa Argentina.

Ufunguzi upya wa makao makuu ya KOnferensi ya Yunioi ya Argentina unaashiria hatua muhimu katika historia ya Kanisa la Waadventista nchini humo, ikithibitisha tena ahadi yake kwa jamii na misheni yake ya utumishi na uinjilisti.

Makala asili ilichapishwa kwenye tovuti ya Kihispania ya Divisheni ya Amerika Kusini.