Southern Asia-Pacific Division

Juhudi za Uinjilisti Zinazoongozwa na Sekretarieti Kusini Magharibi mwa Ufilipino Zasababisha Ubatizo wa Zaidi ya Watu 130

Tangu kuwasili kwa Waprotestanti miaka ya 1970, kumekuwa na ongezeko la waumini wa Kiadventisti katika eneo la Caraga.

Philippines

Washiriki wapya waliobatizwa wanajipanga kwa ajili ya maombi ya kujitolea baada ya sherehe yao ya ubatizo wakati wa mkutano wa injili katika Visiwa vya Dinagat, Ufilipino ya Kusini Magharibi, uliofanyika kuanzia tarehe 17 hadi 21 Aprili, 2024.

Washiriki wapya waliobatizwa wanajipanga kwa ajili ya maombi ya kujitolea baada ya sherehe yao ya ubatizo wakati wa mkutano wa injili katika Visiwa vya Dinagat, Ufilipino ya Kusini Magharibi, uliofanyika kuanzia tarehe 17 hadi 21 Aprili, 2024.

[Picha kwa hisani ya Idara ya Mawasiliano ya SwPUC]

Kwa kuitikia Mpango wa Uhusika Kamili wa Washiriki Wote (Total Member Involvement Initiative, TMI) wa Kanisa la Waadventista Ulimwenguni, Kanisa la Waadventista la Ufilipino ya Kusini Magharibi (SwPUC) lilihamasisha timu yake ya sekretarieti kuongoza kampeni ya uinjilisti katika Visiwa vya Dinagat, iliyopelekea ubatizo wa watu zaidi ya 130 kwenye imani ya Waadventista. Kuanzia tarehe 17 hadi 21 Aprili, 2024, makatibu wa ofisi arubaini na wanane kutoka SwPUC walitekeleza mpango wa uinjilisti katika Visiwa vya Dinagat, sehemu ya mkoa wa Caraga, wakishiriki ujumbe wa matumaini na imani na wakazi wa eneo hilo.

Huku makatibu katika mashirika ya Waadventista wanatambulika kwa umahiri wao na ujuzi wa kitaaluma katika kuhakikisha utendaji kazi usio na itilafu, mpango huu uliangazia kujitolea kwao kushiriki injili kupitia uinjilisti wa umma. Maendeleo haya yanaonyesha ufanisi wa TMI na inasisitiza umuhimu wa ushiriki wa kila mtu katika kushiriki injili kupitia mikakati na maeneo mbalimbali.

"Watu wa eneo hilo ni wenye heshima na wema. Ni wakarimu na wasikivu kwa mahitaji ya wageni wao," Vicky Pamonag, katibu wa ofisi ya SWPUC na mmoja wa wazungumzaji katika hafla hiyo ya wiki moja alisema. Aliongeza kuwa kushiriki katika kampeni za uinjilisti humletea furaha kubwa na kunatoa fursa ya kushiriki upendo wa Mungu na wasioamini. "Lazima nijihusishe katika kazi ya Mungu zaidi ya ofisi. Kushiriki katika kazi hii huleta utimizo wa kiroho katika maisha yangu," aliongeza.

Jumbe za usiku wakati wa kampeni zilishughulikia mada mbalimbali muhimu zinazotambulisha kweli za Biblia, ikijumuisha Sabato, wokovu, hali ya wafu, mbingu, kanuni za vyakula, na ubatizo. Kila mada iliwasilishwa kwa uangalifu ili kushughulikia mahitaji ya kiroho na udadisi wa waliohudhuria.

Mafanikio ya utume ni dhahiri katika idadi ya watu waliochagua kumpokea Yesu kama Mwokozi wao binafsi, jumla ya washiriki wapya zaidi ya 130 ambao wameikubali imani ya Waadventista. Uongofu huu sio tu ushahidi wa nguvu ya ujumbe unaoshirikiwa bali pia nia na ari ya makatibu wa ofisi walioshiriki katika kampeni.

Mpango wa Konferensi ya Yunioni ya Kusini-Magharibi mwa Ufilipino wa kuandaa tukio lenye matokeo kama haya unaonyesha ufanisi wa juhudi za ushirikiano katika uinjilisti. Kujitolea kwa makatibu, pamoja na upokeaji wa wakazi wa Visiwa vya Dinagat, kumesababisha mavuno makubwa ya kiroho, na kuunda jumuiya yenye nguvu ya Waadventista katika eneo hilo.

Kutoka makao makuu ya yunioni yaliyopo katika Jiji la Cagayan de Oro, safari hadi Visiwa vya Dinagat huchukua angalau masaa 11, ikiwa ni pamoja na kivuko. Dinagat ni moja ya jamii za zamani katika eneo la Caraga; ustawi wake unarudi nyuma hadi enzi za kabla ya ukoloni. Jimbo la kisiwa lilikuwa eneo la mapambano ya kihistoria ya Mlango wa Surigao wakati wa Vita vya Pili vya Dunia. Mwaka 2011, Visiwa vya Dinagat rasmi vilikuwa jimbo, vikitenganishwa kutoka Surigao del Norte. Kwa sasa lina idadi ya watu zaidi ya laki moja. Tangu kuwasili kwa Waprotestanti miaka ya 1970, kumekuwa na ongezeko la waumini Waadventista katika eneo hilo.

Makala asili ilichapishwa katika tovuti ya Divisheni Kusini mwa Asia na Pasifiki.