Adventist Development and Relief Agency

ADRA Inachangia Suluhisho za Tabianchi katika COP 28

Shirika la Waadventista linathibitisha azma yake kwa utunzaji wa mazingira kupitia majadiliano, ushirikiano, na miradi inayotekelezwa

Picha: UNclimatechange

Picha: UNclimatechange

Shirika la Maendeleo na Misaada la Waadventista (ADRA) lilikuwa kiongozi muhimu wa kibinadamu katika COP 28, likikuza miradi inayojali mazingira na kusaidia jamii zilizo hatarini kuanzisha mazoea ya kustahimili hali ya hewa. Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, unaojulikana kama COP 28, ulitambua rasmi ADRA kama wakala shirikishi wa kibinadamu wa tukio la kimataifa, lililofanyika Dubai, Falme za Kiarabu, kuanzia Novemba 30–Desemba 12, 2023. Kutambuliwa huku kunaimarisha zaidi hadhi ya ADRA kama taasisi yenye ushawishi inayoongoza miradi ya kijani na kuongeza sauti yake katika mikutano ya baadaye.

Wawakilishi wa ADRA kutoka Marekani, Ujerumani, Uingereza, Kanada na Madagaska walikutana na wajumbe kutoka nchi mbalimbali na washirika wanaoaminika, ikiwa ni pamoja na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (United Nations Office for the Coordination of Humanitarian Affairs, OCHA) na Kurugenzi Kuu ya Ulinzi wa Raia wa Ulaya na Operesheni za Misaada ya Kibinadamu (Directorate-General for European Civil Protection and Humanitarian Aid Operations, DG ECHO). ADRA ilionyesha mbinu zake za jumla za riziki, matumizi endelevu ya ardhi, mbinu za upandaji miti upya, utaalamu wa uhasibu wa kaboni, na mifumo ya chakula.

Picha: UNclimatechange
Picha: UNclimatechange

Kutotabirika kwa tabianchi kuna madhara ya kimataifa, lakini inadhuru hasa katika maeneo yanayokabiliwa na uhaba wa chakula. Zaidi ya watu milioni 333 walitarajiwa kukabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula mnamo 2023, bila kujua mlo wao ujao utatoka wapi.

"Kama shirika la kibinadamu lenye zaidi ya ofisi 100 za nchi zilizounganishwa katika muundo wa jumuiya za wenyeji wanazohudumia, ADRA ina nafasi ya kipekee ya kuzungumza kwa ajili ya wale walio katika hatari kubwa ya hali ya tete ya tabianchi," anasema Imad Madanat, makamu wa rais wa Masuala ya Kibinadamu na Viwango vya Mtandao katika ADRA. "ADRA ilikuwa moja ya mashirika machache tu yaliyokutana na Kamishna Mkuu wa UNHCR Filippo Grandi ili kutetea mahitaji ya watu waliokimbia makazi na jinsi mabadiliko ya tabianchi yataongeza idadi hiyo."

Madanat aliongeza, "Katika Mkutano wa COP 28 Farmers Constituency Meeting, pia tulipata fursa ya kusisitiza umuhimu wa kuzingatia wakulima wadogo na mashamba yanayomilikiwa na wanawake kwa sababu ndiyo yameathiriwa zaidi na athari mbaya za hali mbaya ya tabianchi."

Wajibu wa ADRA katika COP 28

Katika COP 28, ADRA ilishiriki katika majopo kadhaa na kuandaa vikao vya mada, ikiwa ni pamoja na kimoja kilichoitwa "Uhasibu wa Carbon kwa Watendaji wa Kibinadamu,Carbon Accounting for Humanitarian Actors" ambacho kilishughulikia majukumu ya kibinadamu kufanya shughuli zinazoathiri mazingira. Wanajopo wanaowakilisha mashirika ya kibinadamu, mashirika ya serikali, na wataalamu wa mazingira waligundua jinsi biashara na taasisi zinavyoweza kutumia kikokotoo cha kaboni kupima athari zao kwa mazingira na kuendeleza miradi ya kupunguza uzalishaji wa kaboni kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

Mnamo 2022, ofisi za ADRA kutoka Ujerumani na Kanada zilishiriki katika Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (International Committee of the Red Cross, ICRC) na mradi wa majaribio wa EcoAct ili kuunda Kikokotoo cha Kibinadamu cha Carbon. Mpango huo ulisaidia ADRA katika kukokotoa uzalishaji wa gesi chafuzi kutoka kwa miradi katika sehemu mbalimbali za dunia.

"Kuzungumza kuhusu uhasibu wa kaboni ina maana kwamba tunataka kuwajibika kwa matendo yetu wenyewe, na tunataka kuhakikisha kuwa jumuiya tunazohudumia pia zinastahimili hali ya hewa katika siku zijazo. Ofisi za mtandao wa kimataifa wa [ADRA] ni sehemu ya muundo wa jumuiya za wenyeji; ina maana tunahitaji kuchukua hatua, tunahitaji kuwa wa kijani, na tunahitaji kuwa endelevu zaidi. Kwa hivyo tunajivunia kuwa sehemu ya mjadala huu muhimu,” anasema Carina Rolly, msimamizi wa jopo na utetezi na mshauri wa sera wa ADRA Ujerumani.

ADRA iliandaa mjadala kuhusu "Mifumo Inayostahimili na Jumuishi ya Chakula: Kuimarisha Marekebisho ya Hali ya Hewa kwa Usalama wa Chakula na Lishe Ulimwenguni" na Welthungerhilfe na World Vision. Kongamano la watoa maamuzi na wawakilishi kutoka vikundi mbalimbali vya vizazi vilichunguza jinsi uharibifu wa mazingira unavyoongeza hatari ya utapiamlo miongoni mwa watu walio hatarini.

ADRA pia ilishiriki katika kikao cha "Mishtuko Inayosababishwa na Tabianchi na Mwitikio wa Kibinadamu yaani Climate-Induced Shocks and Humanitarian Response" ili kusisitiza asili ya muunganiko wa usalama wa chakula, mabadiliko ya tabianchi, na juhudi za kibinadamu. Majadiliano hayo yalisisitiza hitaji muhimu la mawazo mapya na njia shirikishi kwa ajili ya mipango muhimu ya kitamaduni, inayozingatia hali ya hewa ambayo inawawezesha wanawake, wasichana na familia kujenga jumuiya salama, zenye usawa, na zinazostahimili.

Picha: UNclimatechange
Picha: UNclimatechange
Mbinu za Tabianchi-Thamin (Climate-Smart) za ADRA

ADRA iko mstari wa mbele katika kupambana na uharibifu wa mazingira unaosababishwa na mabadiliko ya tabianchi. Ushiriki wa shirika la misaada ya kibinadamu katika COP 28 na mikutano ya kilele ya siku zijazo huliruhusu kuendelea kushiriki masomo yaliyopatikana na mbinu bora zaidi. Wasaidizi wa kibinadamu wa ADRA wana utaalamu wa kuleta mazingatio kwa masuluhisho kwa idadi ya watu walioathiriwa na hali ya hewa kwa vile shirika limetekeleza miradi ya kukabiliana na hali ya hewa ambayo imesaidia jamii ambazo hazijahudumiwa duniani kote kwa zaidi ya miaka 40. Mipango ya ADRA ya kijani ni pamoja na mifumo ya umwagiliaji inayostahimili ukame, makao yanayostahimili magonjwa, nyumba za kuhifadhi mazingira, miradi ya kulisha shuleni ili kuboresha lishe ya watoto, na mbinu za kilimo rafiki kwa mazingira.

Wito wa Kuchukua Hatua wa ADRA

Picha: UNclimatechange
Picha: UNclimatechange

ADRA inahimiza jumuiya za asili zote kujiunga na mpango wa #GoGreenWithADRA na kushiriki katika shughuli za urafiki wa mazingira zinazorembesha vitongoji vya karibu. Gundua mifumo ya ADRA kwa kupanda miti na ujifunze jinsi shule na vijana wanavyoshiriki katika shughuli za elimu kwa lengo la kulinda jamii dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi.

The original version of this story was posted on the ADRA website.