Mid-America Union Conference

Yunioni ya Waadventista ya Amerika ya Kati Wazindua Ufadhili wa dolla 40,000 kwa Wanafunzi wa Chuo Kikuu wa Mwaka wa Kwanza

Tuzo hii mpya itawapa jumla ya wanafunzi 10 wa mwaka wa kwanza wa theolojia, elimu, uhasibu, na IT hadi dola 40,000 kuelekea gharama za elimu kwa miaka minne na kazi iliyothibitishwa katika huduma ya wakati wote katika kanisa la Waadventista baada ya kuhitimu.

Yunioni ya Waadventista ya Amerika ya Kati Wazindua Ufadhili wa dolla 40,000 kwa Wanafunzi wa Chuo Kikuu wa Mwaka wa Kwanza

[Picha: Jarida la Outlook]

Mwajiri mwenye ari anawapa wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Waadventista cha Yunioni hadi dola 40,000 katika ufadhili wa masomo na kazi ya uhakika baada ya kuhitimu. Mwajiri huyo ni Konferensi ya Yunioni ya Amerika ya Kati ya Waadventista Wasabato. Tuzo hii mpya itawapa jumla ya wanafunzi 10 wa mwaka wa kwanza wa theolojia, elimu, uhasibu, na IT hadi dola 40,000 kuelekea gharama za elimu kwa miaka minne juu ya masomo ya mahitaji ya sasa na masomo ya kitaaluma ya chuo kikuu - na inakuja na kazi iliyothibitishwa katika huduma ya wakati wote katika kanisa la Waadventista baada ya kumaliza digrii zao.

"Tunafahamu kwamba kuna vijana katika makutaniko yetu ambao wanahisi wameitwa kuendeleza kazi ya Injili," alisema Gary Thurber, rais wa Yunioni ya Amerika ya Kati na mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Chuo Kikuu cha Union Adventist. “Wachache mno kati yao wana uhuru wa kifedha wa kufuata shauku yao ya huduma ya kanisa.”

Baadhi ya wanafunzi wanahisi wamenaswa katika mtego wa kifedha. Ikiwa wataacha chuo, hawatajifunza ujuzi ambao kanisa linahitaji. Ikiwa watachukua mikopo mingi ya wanafunzi, shinikizo la kulipa linawalazimisha kuingia katika ulimwengu wa makampuni badala ya kujiunga na huduma.

Thurber anaamini kuwa Kanisa la Waadventista Wasabato linakabiliwa na njia panda na linahitaji kuchukua hatua sasa kuhakikisha kuna wachungaji, walimu, wataalamu wa IT, na wahasibu wa kutosha tayari kuhudumu katika miaka ijayo.

"Kufadhili udhamini huu ni uwekezaji katika siku zijazo za kanisa la Waadventista," alisema.

Wanafunzi hadi kumi wa mwaka wa kwanza watachaguliwa kupokea Ufadhili huu wa Ajira wa Kanisa la merika ya Kati katika muhula wa msimu wa vuli wa mwaka wa 2024. Waombaji lazima wakubaliane na:

  • Kushiriki kikamilifu katika programu ya masomo inayoelekea kwenye shahada ya uhasibu, sayansi ya kompyuta, elimu au theolojia.

  • Kufanya kazi kampasini na kuweka sehemu ya mapato yao kwenye bili ya ada ya shule.

  • Kufanya kazi kama mwanagenzi katika shirika la Waadventisa la Amerika ya Kati.

  • Wakubali kuhudumu kwa angalau miaka minne katika kanisa la Waadvenista la Amerika ya Kati, shule au shirika la uongozi wa kikanda.

Katika fani zote zinazostahiki kupata ufadhili huu, Chuo Kikuu cha Union Adventist kinatoa programu zenye nguvu zinazopewa kipaumbele cha uzoefu wa dunia halisi na huduma. Kwa mfano, programu ya maandalizi ya uchungaji ya chuo kikuu inawajumuisha wanafunzi katika huduma za makanisa ya mitaa mapema zaidi katika mafunzo yao kuliko vyuo vikuu vingine vingi. Kila mwanafunzi wa mwaka wa mwisho pia anapata uzoefu wa muhula maalum kama mchungaji msaidizi chini ya ulezi wa mchungaji mkuu ambapo wanazama katika kila nyanja ya kuongoza kusanyiko.

Wanafunzi wa elimu wana faida ya kujifunza katika Shule ya George Stone, darasa la viwango vingi lililopo kampasini. Wanafunzi wa chuo kikuu huchunguza na kufundisha katika shule ya msingi kuanzia mwaka wao wa kwanza, kuhakikisha kuwa uzoefu wao wa kazi unaanza muda mrefu kabla ya mwanafunzi wao mkuu kufundisha.

Kwa wahitimu wakuu wa uhasibu, kuchukua zamu zinazotoa usaidizi wa kuandaa ushuru bila malipo katika Kituo cha Ujirani Mwema huwaonyesha thamani ya ujuzi wao wa kitaaluma na uwezo wao wa kutumika katika huduma.

"Inafurahisha kukutana na mwanafunzi wa baadaye ambaye ana shauku ya huduma na utumishi," Ryan Teller, makamu wa rais wa Yunioni wa usimamizi wa usajili. "Ufadhili huu unatupa njia mpya ya kuunganisha mambo kati ya fedha zao na ndoto zao. Tunashukuru kwa uongozi wa Yunioni ya Amerika ya Kati tunapofundisha kizazi kijacho cha wafanyakazi wa kanisa."

Ili kujifunza zaidi kuhusu udhamini, tembelea uau.edu/mid-america-scholarship.

Makala asili ilichapishwa kwenye tovuti ya habari ya Yunioni ya Amerika ya Kati, Jarida la Outlook.