South Pacific Division

Waziri Mkuu wa Tonga Ashukuru Kanisa la Waadventista

Wakati wa ziara yake, Ted Wilson, Rais wa Konferensi Kuu, alishiriki katika tukio la mavuno la Tonga 4 Christ ambapo watu 122 walibatizwa.

Waziri Mkuu wa Tonga Hu’akavameiliku Siaosi Sovaleni pamoja na Ted Wilson.

Waziri Mkuu wa Tonga Hu’akavameiliku Siaosi Sovaleni pamoja na Ted Wilson.

[Picha kwa hisani ya: PM Press]

Mnamo Mei 15, 2024, Hu’akavameiliku Siaosi Sovaleni, Waziri Mkuu wa Tonga, alieleza shukrani zake kwa Kanisa la Waadventista Wasabato wakati wa mkutano na Ted Wilson, Rais wa Konferensi Kuu (GC).

Waziri Mkuu alitoa shukrani kwa niaba ya watu wa Tonga na serikali kwa msaada wa kibinadamu unaoendelea na msaada wa ujenzi uliotolewa baada ya majanga ya asili, ikiwa ni pamoja na mlipuko wa volkano ya Hunga Tonga-Hunga Ha’apai mwaka 2022.

Pia alisisitiza juu ya dhamira thabiti na maadili ya pamoja, hasa katika sekta za elimu na afya.

Waziri Mkuu wa Tonga pamoja na Mchungaji Wilson, mkewe Nancy na viongozi wengine wa kanisa.
Waziri Mkuu wa Tonga pamoja na Mchungaji Wilson, mkewe Nancy na viongozi wengine wa kanisa.

Waziri Mkuu alipongeza ziara ya Wilson na kusisitiza jukumu kubwa ambalo taasisi za kidini na serikali zinafanya katika kuimarisha uhusiano na kukuza ushirikiano.

Akijibu, Wilson alitoa shukrani zake kwa Waziri Mkuu kwa kupata fursa ya kukutana na kujadili maeneo kwa ajili ya ushirikiano zaidi.

Ziara ya Wilson ilithibitisha azma ya kanisa katika kuendeleza uelewa na kujenga mahusiano ya kudumu duniani kote.

Mkutano wa rais wa GC na Waziri Mkuu ulikuwa miongoni mwa ratiba iliyosheheni mikutano na shughuli mbalimbali kwa Wilson wakati wa ziara yake nchini Tonga kuanzia Mei 13 hadi 16. Pia alikutana na Mfalme Tupou VI na Malkia Nanasipau’u, alizindua ofisi mpya ya Misheni ya Tonga, alihudhuria kiamsha kinywa cha maombi, na alishiriki katika tukio la mavuno la Tonga 4 Christ katika Chuo cha Waadventisa cha Beulah, ambapo watu 122 walibatizwa.

Baada ya kuondoka Tonga, alisafiri hadi Fiji kwa matukio zaidi, ikiwa ni pamoja na sherehe ya ufunguzi katika Chuo Kikuu cha Waadventisa cha Fulton.

Rais wa Divisheni ya Pasifiki Kusini Glenn Townend na Ted Wilson katika mkutano na Waziri Mkuu.
Rais wa Divisheni ya Pasifiki Kusini Glenn Townend na Ted Wilson katika mkutano na Waziri Mkuu.

Makala asili ilichapishwa kwenye tovuti ya habari ya Divisheni ya Pasifiki Kusini, Adventist Record.