Inter-European Division

Wawasiliani Waadventista wanajadili Misheni ya Kidijitali nchini Ujerumani

Washiriki arobaini kutoka katika vituo 13 vya habari barani Ulaya walikutana katika Hope Media Europe kujadili mawasiliano ya kidijitali na misheni.

Washiriki 40, wanaotoka vituo kumi na vitatu vya barani Ulaya , walikutana mnamo Februari 24-27,2023, kwenye majengo ya Hope Media Europe , huko Alsbach-Hahnlein,Ujerumani . Katika siku nne za mkutano ,washiriki walipata fursa ya kuwasilisha uhalisia na miradi yao mahususi kwa siku zijazo,kubadilishana uzoefu kwa changamoto zao,na kutafuta njia mpya za misheni kwa njia ya mawasiliano.

“Madhumuni ya mkutano huu yalikuwa kuweka mawasiliano ya karibu,na kwa matumaini kwa msingi wa kudumu,wale wanaohusika na vituo vya vyombo vya habari katika eneo la kitengo cha Kimataifa cha Ulaya [EUD],wakijiunga na baadhi ya idara ya Trans-Ulaya[TED],’’alieleza Paulo Macedo,mkurugenzi wa Mawasiliano wa EUD. “Hakukuwa na kongamano rasmi katika ngazi hii na wao kubadilisha taarifa na uzoefu,kuratibu miradi ,kutafuta jukwaa la pamoja la kutimiza dhamira hiyo kupitia vyombo vya habari pamoja.Na ndiyo maana tumekutana hapa na sasa’’

Vyombo vya habari vinavyowakilishwa vilitoka katika Nyanja za EUD za Austria,Bulgaria,Ufaransa,Ujerumani,Italia,Ureno,Romania,na Uhispania;na kutoka nyanja za TED, wawakilishi kutoka Uingereza,Iceland,Ireland, na Latvia, walikuwepo.Mwalikwa maalum alikuwa Maksym Krupskyi, mkurugenzi wa kituo cha vyombo vya Habari nchini Ukraine.

Mpango wa Sabato

Mario Brito,rais wa EUD,alianza sabatokwa ibada ya Vespers juu ya mada “Kusudi Halisi katika kuwasiliana’’ kulingana na Ezekiel 47 na Yohana 17.

“Ujumbe wenye nguvu Zaidi wakati mwingine haujaandikwa au kusemwa.Tunasoma watu huku wakitusoma,’’Brito alisema.

“Fikiria nia yako unapowasiliana.Ni kutoa taarifa tu?Je,ni kusambaza tu kile unachofikiria ni ujumbe sahihi?Au ni kweli kubadilisha maisha ya watu?

Tafuta mawasiliano yanayoleta tumaini na uzima kwa watu kupitia kristo.Kisha unaweza kushirikiana na Roho mtakatifu kubadilisha maisha ya watu , kama vile maji yanayotoka hekaluni na kuleta uzima katika kitabu cha Ezekieli.’’

Asubuhi ya sabato,David Neal ,mkurugenzi wa mawasiliano wa TED, aliwasilisha mahubiri maalum juu ya tumaini liliopo katika maandiko ya Paulo katika 1Watesalonike 5.

“Watu wa Mungu wamekesudiwa kuleta tumaini kwa ulimwengu ulio katika shida ya kudumu ya ulimwengu na kwa watu walio katika shida kubwa .Tumaini hili linakuwa kusudi letu kwa sababu Mkristo anaishi maisha ya kusudi ,ambayo tunapata msalabani,ndani na kupitia yale ambayo Kristo ametufanyia .Kwa sababu tumaini limepachikwa katika DNA ya Waadventista , tunapaswa kutenda na kuishi kama kanisa tarajio lililo tayari kwa kurudi kwa Kristo na, kama kanisa la Thesalonike,tuwe kanisa la furaha , la maombi, nala shukrani lililowekwa katika neema,’’Neal alisisitiza.

MAONI

Florian Ristea , mkurugenzi wa EUD Adventist Mission, shule ya sabato na Huduma za Kibinafsi , alithibitisha kwamba “ilikuwa kwa kutia moyo kuona watu , hasa viongozi vijana,kutoka kote Ulaya wakijitolea na kuzingatia misheni na kutumia ubunifu na raslimali zao katika kuunda maudhui ya kufikia watu katika nchi zao wakiwa habari njema.Vyombo vya habari ni chombo chenye nguvu ,na ni dhahiri kwamba wakati umefika wa kuwa [kama bado haujawa]nguvu inayoongoza katika misheni ya kanisa.

“Vituo tofauti vya habari vinajikuta katika hatua tofauti tofautiza maendeleo ya kazi zao za huduma ya vyombo vya habari.Kuja pamoja kama mtandao wa Hope media Europe huwezesha vituo vya habari sio tu kwa kukua pamoja kwa kujifunza kutoka kwa kila mmoja lakini pia kuunda mkakati wa pamoja wa wizara ya habari ambao utaongeza athari za vituo vya habari ambao utaongeza athari za vituo vya habari vya umoja na vile vile vya mtandao wote,’’ alisema Klaus Popa ,rais wa Hope Media Europe ,kituo cha vyombo vya habari cha Divisheni ya Inter-European.

“Kulikuwa na habari nyingi njema kuhusu kila kitu ambacho kimefanywa katika misheni kupitia mawasiliano barani Ulaya ,pamoja na mawazo ya kuahidi ,mipango, na miradi ya siku zijazo.Kujifunza ,kushiriki, na kuratibu kutaokoa raslimali na kuhakikisha wakati katika madhumuni yetu ya pamoja,’’Macedo alisema. “ Angalia tu ujumbe wa matumaini kutoka kwa kituo cha habari cha Ukrain.’’

“Hutahitaji mkate au nguo ikiwa utapoteza matumaini kabisa ya kuishi.Tupo kwa ajili ya kuishirikiỊ’’

Wakati wa mkutano wa kituo cha media ,EUD na TED News walihojiana na Maxim Krupski,mkurugenzi wa Hope Media Ukraine.

“Kwanza, waliona watu wakiteseka na kuondoka,na tulifikiri kila kitu kimepotea,’’alishiriki Krupski katika mahojiano yaliyofanyiwa na Vanesa Pizzuto,mkurugenzi mshiriki wa TED communications ,na Samuel Gil mkurugenzi wa Hope Media Hispania.“Kisha tukaanza kusaidia watu[na]mahitaji yao ya kimsingi na muhimu.Mara tu baada ya miezi michache ya kwanza ya vita,tulitambua kwamba kuna fursa ya kueneza injili.Watu wanahitaji matumaini ya kuendelea kutaka kuishi.’’

Krupski alionyesha mwanga machoni pake,akitokwa kwa hisia za kuzungumza juu ya mateso katika nchi yake na furaha ya kutangaza habari njema katikati ya dhiki na kutokuwa na uhakika.“Tayari tumekuwa na ubatizo Zaidi ya 1000 tangu mwanzo wa vita hivi vya kutisha ,’’aliarifu.“Na tulizindua studio mpya katika msimu wa joto,’’alitangaza kwa furaha.“Kama ungeniambia tungezindua studio,hata kabla ya vita , nisingeamini.’’

Ukraini inakabiliwa na matokeo mabaya ya ghasia na ufukara kwa mwaka mzima.Katika ngazi ya kanisa,waumini 8,000 ya 30,000 wameondokanchini.Hata hivyo ,misheni inaendelea na kukua na wafanyikazi 100 wanaofanya kazi katika studio saba za Hope Media Ukraini.

“Tunawashukuru wote kwa kuunga mkono watu wetu na wanachama wetu.Tunafanya misheni inavyohitajika,’’alihitimisha Krupski.

The original version of this story was posted on the Inter-European Division website.