Inter-American Division

Waadventista Wanasherehekea Miaka 10 ya Kueneza Matumaini Kupitia Kituo cha Televisheni cha Kifaransa

Espérance TV InterAmérique inaendelea kusambaza ujumbe wa wokovu kwa maeneo yanayozungumza Kifaransa duniani kote.

Waadventista Wanasherehekea Miaka 10 ya Kueneza Matumaini Kupitia Kituo cha Televisheni cha Kifaransa

[Picha: Divisheni ya Baina ya Amerika]

Waadventista Wasabato katika eneo la Yunioni ya Antilles Guiana ya Ufaransa hivi majuzi walisherehekea miaka 10 ya kueneza ujumbe wa injili kupitia Espérance TV Interamérique wakati wa sherehe maalum. Idhaa hiyo ya Kifaransa ni mojawapo ya chaneli tatu za televisheni chini ya Hope Channel Inter-America inayoendeshwa na Divisheni ya Baina ya Amerika.

Maelfu ya watu walikusanyika katika kanisa la Waadventista la Mount Sinai huko François mnamo Juni 15, 2024, kwa maombi na ibada ya hatua hiyo muhimu iliyofikiwa hadi sasa.

Mchungaji Eddy-Michel Cardin, rais wa Yunioni ya Antilles Guiana ya Ufaransa anawahutubia washiriki wa kanisa katika Kanisa la Waadventista la Mount Sinai huko François, Martinique, wakati wa maadhimisho ya miaka 10 ya kuanzishwa kwa sherehe ya Espérance TV InterAmérique mnamo Juni 15, 2024.

"Leo tumekua pamoja katika imani kwa neema ya Mungu katika utume huu wa kueneza maadili ya Yesu na hasa kueneza ujumbe wenye changamoto wa Malaika Watatu wa Ufunuo 14," alisema Eddy-Michel Carpin, rais wa Yunioni ya Antilles Guiana ya Ufaransa. “Espérance TV imegusa maisha ya watu wengi huko Martinique, Guadeloupe, Guiana ya Ufaransa, na kwingineko katika ulimwengu unaozungumza Kifaransa.” Ulimwengu wa leo unahitaji uhakika unaopatikana katika ahadi iliyotolewa na Bwana wetu Yesu, aliongeza Carpin.

Carpin alitoa changamoto kwa viongozi wa chaneli hiyo na wafanyikazi wa utayarishaji kuweka upya juhudi zao na akahimiza kujitolea upya katika kupanua programu zaidi zinazoweza kuwasogeza watazamaji maisha bora hapa duniani na kwa ajili ya uzima wa milele.

Mchungaji Eddy-Michel Cardin wa Yunioni ya Antilles Guiana ya Ufaransa anawahimiza viongozi na washiriki kuendelea kujitolea na kujizatiti katika kupanua kituo cha televisheni ili kuwafikia watazamaji wengi zaidi na ujumbe wa matumaini.

Iliyoko Martinique, kwenye majengo ya ya Yunioni ya Antilles Guiana ya Ufaransa huko Forte-de-France, Espérance TV InterAmérique huendesha vipindi 24/7 vinavyoangazia mada kuhusu afya, elimu, familia, watoto, vijana, pamoja na semina na zaidi.

Esperance TV imekuwa na changamoto, ushindi, na ukuaji wa mara kwa mara, alisema Claudine Ténitri, mkurugenzi wa Espérance TV InterAmérique.

Ténitri aliwashukuru wasimamizi na viongozi wa kanisa ambao walisaidia sana kuanzisha chaneli hiyo mwaka wa 2014 na wameisaidia kuwa kama ilivyo leo.

Claudine Trénite, mkurugenzi wa Espérance TV InterAmérique, anamshukuru Mungu kwa neema yake tangu mwanzo ambapo kituo cha televisheni kilianza kupeperusha vipindi mwaka wa 2014.
Claudine Trénite, mkurugenzi wa Espérance TV InterAmérique, anamshukuru Mungu kwa neema yake tangu mwanzo ambapo kituo cha televisheni kilianza kupeperusha vipindi mwaka wa 2014.

“Ni vigumu kuzungumzia safari yetu bila kukiri uingiliaji kati wa Mungu ambao umeongoza kila hatua katika njia yetu," alisema. “Tangu siku ya kwanza, Mungu amekuwa dira yetu, chanzo chetu cha msukumo. Ni kwa hekima Yake kwamba maono ya Esperance TV yaliundwa, na ni kwa rehema zake tuliweza kushinda vizuizi, na kubadilisha kila shida kuwa ukuaji na fursa mpya.

Katika kuwashukuru wasimamizi wa zamani na wa sasa, wafanyakazi wa uzalishaji, na wafanyakazi wa kujitolea, Ténitri alisema: “Msaada wenu usio na masharti, ukarimu wenu linapokuja suala la wakati na vipaji pamoja na maombi yenu ya kila mara yamekuwa muhimu kwa misheni yetu.” Aliwashukuru kwa moyo wao wa jumuiya na huduma ya kujitolea, kuruhusu Espérance TV kuangaza zaidi ya matarajio ya awali. "Kazi yenu ngumu, mara nyingi kwenye kivuli, na ubunifu wenu umekuwa injini nyuma ya ufikiaji wetu," alisema. "Kila programu, kila nugget inayotangazwa ina alama ya kujitolea na ubora," aliongeza.

Viongozi wa kanisa wakipiga picha baada ya kipindi maalum kurushwa moja kwa moja kusherehekea maadhimisho ya miaka 10 ya kituo hicho.
Viongozi wa kanisa wakipiga picha baada ya kipindi maalum kurushwa moja kwa moja kusherehekea maadhimisho ya miaka 10 ya kituo hicho.

Ténitri alishukuru watazamaji kwa kuwa moyo wa kituo hicho. “Uaminifu wenu, maoni yenu ya kuhamasisha na utazamaji wenu wa kudumu unatuhamasisha kupita mipaka yetu kila siku. Ninyi ni washirika wetu katika misheni hii ya kutangaza matumaini na maarifa ya kibiblia katika kila kipindi kilichoonyeshwa.” Aliendelea kwa kuwatia moyo viongozi na washiriki kushirikiana katika kujenga zaidi ya kituo cha televisheni.

"Tumeunda nafasi ya kushiriki, kutafakari, na ambapo nuru takatifu inaangazia kila programu na kila uingiliaji kati," Ténitri alisema.

Mtayarishaji Mkuu wa Hope Channel Inter-America, Abel Márquez, anasifu kazi ya kujitolea ya viongozi na watayarishaji wa vyombo vya habari kwa kufanya kituo cha Kifaransa kuwa taa ya matumaini kwa ulimwengu.

Abel Márquez, Mkurugenzi Mtendaji wa Hope Channel Inter-America, alisifu kazi iliyotolewa kwa bidii katika kuikuza kituo cha Kifaransa kuwa mwanga wa matumaini kwa ulimwengu. “Tunajiunga nanyi katika miaka hii 10 ya ukuaji na zaidi kusherehekea kile mafanikio haya yanamaanisha katika juhudi zenu za kutimiza misheni ya kushiriki matumaini,” alisema Márquez. “Kama sehemu ya Mtandao wa Hope Channel Inter-America, tunatazamia siku za usoni kwa uhakika kwamba juhudi zenu zitaendelea kuwa baraka kwa maelfu ya watu katika eneo letu linalozungumza Kifaransa na zaidi ya hapo.”

Espérance TV InterAmérique inapeperushwa kupitia esperancetv.org na Chaneli ya YouTube ambao una zaidi ya wajisajili 10,000 na pia unasambazwa kupitia hopechannelinteramerica.org na majukwaa ya kidijitali kama Roku, Hope Channel na mengineyo. Kituo hiki kinashiriki vipindi kutoka Canada na Ufaransa kupitia makubaliano maalum na Hope Channel International.

Makala asili ilichapishwa kwenye tovuti ya Divisheni ya Baina ya Amerika.