Waadventista Kule Thailand Wageuza Mkahawa kuwa Mahali pa Kuabudu

Southern Asia-Pacific Division

Waadventista Kule Thailand Wageuza Mkahawa kuwa Mahali pa Kuabudu

Mbinu ya uinjilisti isiyo ya kawaida ni sehemu ya mpango wa Kristo kwa Thailand unaofanyika katika zaidi ya maeneo 30 katika eneo lote.

BANGKOK, Thailand- Kundi la washiriki kutoka kanisa la Kiadventista la Trinity lilianza mpango maalum wa kueneza injili kwa kuwa na mikutano, si kanisani, bali katika mkahawa ulioko katikati mwa wilaya ya Pratunam kule Bangkok. Kinachoshangaza, usimamizi ulitoa kibali cha kufanya mkutano wiki nzima katika majengo yao. Kikundi hiki na mikutano yao ya usiku ilikuwa kwa uungwaji mkono wa Yesu kwa WanaThailand uliyofanyika katika maeneo 30 nchini.

Washiriki walipanga mpangilio huo kila usiku, wakionyesha nyimbo mabalimbali, vipindi vya afya, ujumbe za kutia moyo kwa watu wanaoizuru na kutoka mkahawa ule. Mikusanyiko ya mikutano ilikuwa machi, 1-6, 2023.

“Tunataka kuwafikia watu mahali walipo na kuwanyesha upendo wa yesu,” alisema Mchungaji Nelson Paulo, Mkurugenzi wa Huduma za watu na mambo ya uhuru wa kuabudu wa kanisa la Kiadventista katika divisheni ya Southern Asia- Pacific. Watu wengi wanaogopa kuja kanisani, lakini kwa kushiriki mikutano katika mkahawa, tunatumai kuunda mazingira mazuri mahali watu wanaweza kujihisi huru na kuwakuta wengine katika jamii.

Mkahawa ulihamishwa ukawa kanisa kwa wakati, huku meza na viti vikundwa kwa jinsi ya kupeana nafasi. Kundi hili pia lilizindua hatua za usalama za kuzuia COVID-19, ikiwemo kuvaa barakoa na kusafisha mikono kwa sabuni. Mmiliki wa mkahawa alikaribisha wazo kwani lilileta watu kwa biashara yake na kuanzisha uhusiano mwema kati ya mkahawa na jamii. Mikutano ilileta mawazo ya wakaaji na wageni katika eneo hilo.

“Nilikuwa napita na nikasikia nyimbo,” alisema Mmoja wa wanajamii aliyehudhuria mkutano. “Ilikuwa ya kupendeza na kuinua roho. Ilibidi niingie ndani na kuona kinachotendeka.”

Mbinu hii maalum ya kuuhubiri ilipokea mtazamo kutoka kwa jamii kubwa ya waadventista, huku wengine wakipongeza washiriki kwa ujuzi na ukubali wao wa kuwafikia watu wa jamii kwa njia za dunia

“Huu ni mpangilio mzuri unaonyesha ujuzi katika kueneza injili.” Alisema pastor Roger Caderma, Rais wa waadventista kule Divisheni ya Asia-Pacific. Natumai kanisa nyingi zitafuata mfano huo na kuzindua njia za kuwajumuisha watu katika jamii

Kanisa la Waadventista la Trinity na washiriki wao wanatumaini kuwa nguvu zao hazitaongoza watu kumjua yesu tu bali pia kuwashawishi washiriki wengine kufikiria mbinu nyingine wakati wa kueneza injili.

The original version of this story was posted on the Southern Asia-Pacific Division website.