Viongozi wa Vyuo Vikuu vya Waadventista Watembelea Hospitali ya Mitaa, Kuombea Wagonjwa

South American Division

Viongozi wa Vyuo Vikuu vya Waadventista Watembelea Hospitali ya Mitaa, Kuombea Wagonjwa

Nje ya Hospitali ya Kitaifa ya Guillermo Almenara Irigoyen, wakuu wa Chuo Kikuu cha Umoja wa Peru, maprofesa, kitivo, makasisi na wasimamizi waliimba nyimbo na kuombea wagonjwa waliokuwa ndani.

Kama vile siku kumi za maombi na saa kumi za kufunga zilikuwa na mada ya “Mungu kwanza” na kuunga mkono kanisa ya kiadventista kule peru kusini, Chuo kikuu cha Peruvian Union kinaongoza kampeni peru inayokuombea. Kwa jinsi hii uongozi na kamati ya afya ya Hospitali ya kitaifa ya Guillermo Almenara Irigoyen kule Lima, hospitali ya pili kwa ukubwa wa usalama wa kijamii kule peru ilijiunga pamoja kuwaombea wagonjwa wanaosumbuka na ugonjwa kila siku. Zaidi, jambo hili lilileta tumaini kwa familia za wagonjwa.

Hospitali ya kitaifa ya Guillermo Almenara Irigoyen ina huduma mbalimbali kama vile: idara ya nje, kuwalaza hospitali, dharura, na kitengo cha kuwahudumia wagonjwa wa hali mahututi na vyumba vya upasuaji. Nje ya hospitali, wasimamizi wa idara, maprofesa na wahubiri na wasimamizi wa chuo waliimba nyimbo huku wakipiga magoti na kumlilia mungu. Wauguzi na madaktari waliguzwa na kitendo hicho cha ujasiri.

“Ni mpangilio mzuri ambao chuo kikuu cha Peruvian union kinafanya, kuleta ujumbe wa mungu ambao tunahitaji sana. Sisi, pamoja na huduma zetu, tuko kwa ajili ya wagonjwa wetu ili kuwapa huduma bora ya afya, na maombi pia ni muhimu,” Alisema Dkt. Emperatriz Santa Cruz Benavente, mkuu wa matibabu ya kina katika hospitali.

Kwa njia hii, ya “Peru inakuombea” kampeni ilikuja kueneza neno la mungu na kuwatuliza wale watoa huduma. “Sisi Wafanyakazi wa Essalud wanaotoa huduma tunahisia na tuna mungu ambaye tunawapa wagonjwa wetu,”Alimaliza Dkt. Benavente.

Mchungaji Eduardo Bailon, Msaidizi wa ushirika katika chuo alisema kuwa kupitia “ peru inakuombea” UpeU imekuwa ikifanya vitendo hivi kwa taasisi mbali mbali nchini. “ Sisi tukiwa baadhi ya taasisi ya Kiadventista, huenda nje kuwazuru jamii, hospitali, maafisa wa polisi na wakuu katika uongozi ili kuwaombea. Ni vizuri kujua kuwa kuna wengine ambao huwaombea, alisema

Zaidi, taasisi nyingi zilizuliwa kule maeneo ya San Martin na Puno, kama vile munisipa za mikoa ya San Martin, Chuo cha uhandisi cha Peru CD Puno, UGEL san Roman, Wanajeshi wa Peru, Askari polisi wa Peru, Manisipa ya San Roma, Chuo cha Uhasibu cha Peru, Hospitali ya Carlos Monge Medrano na Chuo cha usimamizi.

Toleo la asili la hadithi hii lilichapishwa kwenye tovuti ya habari ya Kihispania ya Idara ya Amerika Kusini.

The original version of this story was posted on the South American Division Spanish-language news site.