Huduma ya Vijana Waadventista (Adventist Youth Ministries, AYM) wa Divisheni ya Kusini mwa Asia na Pacific (SSD) ilizindua mpango wa Siku 100 Kwenye Maandiko wa SSD AYM mnamo Agosti 26, 2023, na utafikia kilele tarehe 3 Desemba 2023, wakati wa Kusanyiko la Wasomaji Biblia wa SSD. Mpango huu ulifanywa kwa Kiingereza, Kibahasa, Kivietinamu, Kithai, Kiburma, na lugha zingine chini za SSD.
Mpango huu unatumika kama mwitikio wa kujitolea ili kuimarisha kipengele cha ukuaji wa kiroho ndani ya mfumo wa mpango wa Nitakwenda. Kiashirio kikuu cha utendaji kinajikita katika kuona ongezeko kubwa la ushiriki wa vijana wanaosoma Biblia kwa ukamilifu, kutoka Mwanzo hadi Ufunuo. Mpango huo unajumuisha viashiria vinavyoonekana, vinavyoweza kupimika:
Kutekelezwa kwa Siku 100 kwenye Maandiko Mtandaoni wa SSD na Matukio ya Unioni yote
Ongezeko la Kiasi la Wasomaji wa Biblia Vijana linaloweza Kupimika
Utambuzi Kupitia Vyeti na Pini
Uundaji wa Jumuiya ya Wasomaji Biblia
Kuandaa Mkutano wa Mradi wa Kusoma Biblia
Kudokumenti Mafanikio ya Kusoma Biblia.
Upakiaji wa Video za Kila Siku kwenye Kurasa za Facebook
Vijana wachanga (Adventurers, Pathfinders, and Master Guides), vijana waandamizi (Mabalozi, Wanafunzi wa Huduma ya Kampasi ya Umma, wanafunzi wa AMiCUS, vijana wazima, wataalamu wa vijana, na washauri wa vijana), wasimamizi, na waelekezi husoma Maandiko kila siku saa 5:00 asubuhi. Maombi ya pamoja hufuatia kila somo la Biblia kuziandaa akili za wasomaji na wasikilizaji.
Baadhi ya vijana wameelezea baraka za kujiunga na mpango huu. Sarah L. Homiggop, kutoka Konferensi ya Unioni ya Ufilipino Kaskazini, anashiriki, “Inanileta karibu na Mungu. Ikinifanya kutambua jinsi anavyotuongoza kwa upendo katika kila hatua. Inanishangaza jinsi alivyojibu maombi ya dhati kama vile alivyomjibu mtumishi wake Ibrahimu.”
Quinnie Chua, kutoka Konferensi ya Unioni ya Ufilipino Kusini, anashuhudia, “Baraka ya siku 100 zinazoendelea za Maandiko kwangu ni kwamba ninaweza kuzama katika Neno la Mungu mapema asubuhi ili kuungana Naye tena kila siku—kusoma kila sura nzuri inayotukumbusha ni nani, na mambo ambayo amefanya katika maisha yetu. Ni mahali ambapo tunamjua yeye kwa kina zaidi na jinsi tunavyoweza kuwa baraka kwa watu wengine pia. Hakika ni baraka kwangu kumtumaini yeye kwa maneno yake na kuacha mapenzi yake yatimizwe katika maisha yangu."
Karen P. Monje, kutoka Konferensiya Unoni ya Ufilipino ya Kati, anajibu, “Nimebarikiwa kurejesha kumbukumbu langu kuhusu Biblia. Ninashangazwa na jinsi Mungu anavyovumilia watoto wake wakaidi. Mungu anapaswa kusifiwa na kuabudiwa sasa na hata milele!”
Billy Selintung, kutoka Konferensi ya Singapore, asema, “Kusoma Biblia tena hunikumbusha ahadi nilizopewa. Pia inaeleza juu ya laana na hatari ya kukiuka sheria ya Mungu. Zaidi ya yote, usomaji unaninyenyekeza na unaonyesha jinsi nilivyo dhaifu. Nahitaji kuomba zaidi. Nahitaji kujisalimisha zaidi na kufuata mafundisho ya Mungu. Asante kwa kipindi cha usomaji wa Biblia tulichopewa na huduma yangu.”
Heldha Pandeirot, kutoka Konferensi ya Unioni ya Indonesia Mashariki, anashiriki, “Kujiunga na Siku 100 katika Maandiko kwangu ni ajabu sana. Nimebarikiwa sana, sio kwangu tu bali kwa wanafunzi wangu wa shule ya upili pia. Zaidi ya hayo, hata wanafunzi wasio Waadventista waliathiriwa na tukio hili kuu, na wako tayari kujiona kama wasomaji wa Maandiko pia. Nimeshiriki baraka hii na wanafunzi wangu tangu Mtandao wa Habari za Vijana Waadventista (Adventist Youth News Network) wa EIUC uliponialika kushiriki kama mmoja wa wasomaji. Bwana asifiwe!”
Vicki Kim, kutoka Misheni ya Unioni ya Kusini na mashariki, anashuhudia, “Bwana asifiwe! Mpango huu husaidia kuimarisha imani yangu sana.”
Mo Go, kutoka unioni ya hiyo pia, anashiriki, “Ninafurahia ushirika ninaposoma Biblia pamoja.”
Saw Larry James, kutoka Misheni ya Unioni ya Myanmar (Myanmar Union Mission, MYUM), anashiriki kwa ufupi baraka za Siku 100 katika Maandiko. Anaandika kwa urahisi, "amani."
Lian Sian Huai, pia kutoka MYUM, anaandika, “Programu hii ni baraka sana kwangu kwa njia ambayo kusoma andiko pamoja na vijana wengine hufungua macho yangu kwa kweli ambazo sikuwahi kuona hapo awali. Najisikia furaha sana pia kuona vijana wengi, wengine nawafahamu na wengine siwajui, wakisoma neno la Mungu kwa nia moja kila siku na kubadilishana ufahamu. Ninaamini Mungu angefurahi sana kuona watoto Wake wakifanya hivi. Asante, Mchungaji Ron, kwa kufanikisha hili. Utukufu uwe kwa Mungu.”
SSD AYM inakumbatia usemi wa Yesu: “Mtu hataishi kwa mkate tu, bali kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu” (Mathayo 4:4, NKJV).
Mradi wa usomaji wa Biblia ni sehemu ya Maono ya AYM 2020: “Vijana wenye afya njema ambao wanafurahia uhusiano unaookoa na Kristo, wanapenda Maandiko kama kiwango chao cha kuishi ili kuakisi Tabia kama ya Kristo, kutumikia Kanisa na Jumuiya kwa shauku [au Kampasi. ] wakitumia karama zao za kiroho walizopewa na Mungu, na kutimiza Agizo la injili kwa nguvu katika uwezo wa Roho Mtakatifu.”
The original version of this story was posted on the Southern Asia-Pacific Division website.