Wafanyakazi zaidi ya 100 kutoka Mfuko wa Akiba wa Vanuatu (Vanuatu Provident Fund) wamepokea uchunguzi wa kiafya bila malipo kupitia kampeni ya 10,000 Toes mwezi Agosti.
Kwa baadhi ya wafanyakazi, ilikuwa mara yao ya kwanza kupokea uchunguzi wa kimatibabu, wakiamini kwamba wangefaa kupata uchunguzi huo endapo tu wangeugua.
Iliyowezeshwa na wauguzi wahitimu kutoka Chuo cha Elimu ya Uuguzi cha Vanuatu, Lekon Tagavi, mkurugenzi wa Huduma za Afya za Misheni ya Waadventista ya Vanuatu, na mabalozi wa 10,000 Toes, wafanyakazi walipatiwa ukaguzi wa afya katika sehemu zao za kazi.
Richard Edwin, Meneja Mkuu wa muda wa Vanuatu Provident Fund, aliomba timu ya 10,000 Toes kutoa uchunguzi kwa wafanyakazi wake baada ya kujifunza kuhusu kampeni yao na huduma za uchunguzi wa afya za bure wanazotoa.
Kampeni ya 10,000 Toes, iliyozinduliwa na huduma ya afya katika Divisheni ya Pasifiki Kusini ya Kanisa la Waadventista Wasabato, inalenga kushughulikia tatizo kubwa la magonjwa yasiyo ya kuambukizwa yanayopatikana sana katika Pasifiki Kusini.
Makala asili yalichapishwa kwenye tovuti ya habari ya Divisheni ya Pasifiki Kusini, Adventist Record.