Machi 4,2023,waawake kutoka kanisa za Kiadventista kote ulimwenguni wataungana pamoja ili kuomba kwa ajili ya siku hii ya kimataifa ya Maombi ya wanawake.Watajiombea wao wenyewe,makanisa yao,jumuiya yao,na jumuiya ya kimataifa.Kupitia kwa mada ya mwaka huu, ‘kubadilishwa kupitia kwa maombi,wana kanisa wanaweza kujiunga katika maombi, washiriki pamoja,na waweze kuhimizwa ili wakuze uhusiano wao na Yesu.
NI NINI SIKU YA KIMATAIFA YA MAOMBI YA WANAWAKE
Kitengo cha Idara ya wanawake WM YA Kongamano kuu la Waadventista wa Sabato ilianzisha siku hii maalum ya kila mwaka iliyotengwa kwa ajili ya maombi mwaka 1990.Walitoa wito kwa washiriki wote wa kanisa hilo ,hasa wanawake ,kuonja nguvu ya maombi na furaha ya kusali pamoja.
Katika ulimwengu wa kisasa unaozidi kuwa mgumu na wenye changamoto ,wakurugenzi wa WM wanatambua umuhimu wa kuwa na uhusiano wa kina na wa maana pamoja na Mungu.
Nilde Itin ,mkurugenzi mshirika wa WM anashiriki , ‘sasa kuliko wakati mwingine wowote ,tunahitaji kutumia wakati katika sala kukabiliana na masuala ya ulimwenguni pote,kama vile vita,misiba ya asili,magonjwa na vita vya kiroho.Kuna hitaji la kudumu la kumtegemea Roho Mtakatifu kwa uongozi , hekima, Amani,na nguvu katika maisha yetu ya kila siku tunapokaribia kurudi kwa Yesu haraka.’
Maombi hutuweka katikati na kutukumbusha kwamba hatuko peke yetu na kwamba Mungu anatujali na yuko pamoja nasi daima .Wanawake wa umri na asili zote wamepata faraja katika kushiriki na makanisa yao ya mtaa , au hata mmoja mmoja.
KUBADILISHWA KUPITIA KWA MAOMBI
Kauli mbiu ya mwaka huu , ‘kubadilishwa kwa maombi’ inaangazia jinsi maombi ni mazoezi ya kila siku ambayo yanaweza kubadilisha tabia zetu.Zoezi linalotuleta karibu na Mungu.Kama wafuasi wa Yesu,tumeitwa kuwa kama yeye Zaidi kila siku kwa kumtazama na kutumia muda pamoja naye.Kupitia ushirika huu , Roho Mtakatifu hubadilisha mioyo yetu na kutuwezesha kuakisi vizuri Zaidi sura yake kwa wale wanaotuzunguka.
Itin anasema,Siku iliyoanza kama siku ya kuzingatia maombi kanisani,pia imekuwa ya siku ya kuhama kutoka kanisani hadi kwenye jumuiya ili kuomba na wengine na kuwafikia.Walio hospitalini na wanaohitaji chakula na matunzo’.Anaendelea ,athari yake inaweza kuonekana kwa idadi ya shughuli ,matukio, na fursa ambazo siku hii zimetoa makanisa ya mahali pamoja kuleta watu pamoja, kukuza maisha yao ya maisha yao ya maombi ,lakini wakati huo huo , kuwawezesha kufikia jamii katika njia mbalimbali.
Maombi si ya siku moja tu bali ya kila siku.Nguvu zake zinaweza kubadilisha maisha na matendo yetu,na ulimwengu unaotuzunguka.
JINSI YA KUHUSIKA
Siku ya Kimataifa ya Maombi ya Wanawake inapokaribia ,wote wanaweza kushiriki.Wanaume na watoto pamoja .Wote mnakaribishwa kuomba kwa ajili ya mabadiliko, kwa ajili yao wenyewe na kwa ajili ya wengine. WM pia inawaalika washiriki kuombea mahitaji maalum ,masuala, na changamoto.Katika siku hii ,washiriki wanaweza kukusanyika ili kuombea ulimwengu , familia zao, marafiki , na jumuiya .Wanaweza kusali kwa ajili ya wale wanaohangaika ,wagonjwa, wapweke , au wanaotafuta tumaini.
Makanisa yanaweza kufanya ibada maalum ya sabato ili kusisitiza mada ya mwaka huu.WM inawahimiza washiriki kuhama kutoka kanisani hadi kwenye jumuiya zao, kwa kuwa mikono na miguu ya Yesu.Wanaweza kuwafikia wale walio karibu nao na kushiriki upendo wa Yesu kupitia matendo ya wema na upendo.
Watu binafsi na makanisa wanaweza kupata ubunifu na shughuli za siku hii.Wanaweza kupanga matembezi ya maombi ,kuandaa kifungua kinywa cha maombi ,mkesha wa maombi au kongamano la maombi la wikendi.Uwezekano hauna mwisho.Jambo la muhimu Zaidi ni kwamba wote wakutane katika maombi.
WM hutoa pakiti ya raslimali kwa mada ya kila mwaka.Pakiti hii ina muhtasari wa huduma takatifu,marejeleo ya maandiko ,muhtasari wa program,hadithi ya watoto,mahubiri yaliyoandikwa na semina .Pia inajumuisha slaidi za Powerpoint kwa mahubiri na semina na inapatikana katika lugha Zaidi ya 15.
Kifurushi cha nyenzo cha WM cha kubadilishwa kwa maombi kinapatikana hapa.Ni zana muhimu kwa makanisa ,viongozi , na watu binafsi kutumia wakati wa tukio hili au kujitayarisha kibinafsi.
Tunapojiandaa kwa Siku ya Maombi ya Wanawake 2023,tukumbuke nguvu ya Maombi .Ina uwezo wa kutubadilisha sisi,familia zetu na jamii zetu.Tuungane kwa umoja .Kuinua sauti zetu katika maombi.Kutafuta mwongozo wa Mungu.Kujisalimisha kwa Kristo ili tuishi maisha yaliyogeuzwa.
Kwa wale wanaopenda kushiriki au kujifunza Zaidi kuhusu Siku ya Kimataifa ya Maombi ya Wanawake , au kwa habari Zaidi kuhusu Huduma za Wanawake,tembelea https //women.adventist.org/