South Pacific Division

Safari ya Siku 100 za Maombi Yazinduliwa nchini Papua New Guinea

Mpango wa maombi unatanguliza mpango wa uinjilisti wa Papua New Guinea kwa ajili ya Kristo utakaoanza tarehe 26 Aprili 2024

[Picha imetolewa na Divisheni ya Pasifiki Kusini]

[Picha imetolewa na Divisheni ya Pasifiki Kusini]

Misheni ya Yunioni ya Papua New Guinea (Papua New Guinea Union Mission, PNGUM) imezindua safari ya maombi ya siku 100 kabla ya mpango wa uinjilisti wa PNG for Christ.

Wito huo wa maombi unafuatia machafuko ya hivi karibuni ya kiraia na ghasia nchini humo. “[Siku 100 za maombi] ni mkakati wa kuhamasisha nchi nzima katika kutafuta ulinzi na mwongozo wa Bwana katika utoaji wa PNG for Christ na mipango ya kliniki kubwa ya afya,” alisema rais wa PNGUM Mchungaji Malaki Yani.

Mchungaji Yani alisema kwamba taratibu zimewekwa ili kusimamia usalama wa wazungumzaji wote wa kimataifa. Viongozi wanabainisha kwamba ghasia za kikabila zilitokea katika eneo la PNG ambalo hakuna wazungumzaji wa kimataifa watakaokwenda. Zaidi ya wahubiri 200 kutoka maeneo mbalimbali ya Divisheni ya Pasifiki Kusini wanashiriki katika mpango wa PNG kwa Kristo (PNG for Christ), ambao unaendeshwa kuanzia Aprili 26 hadi Mei 11. Kabla ya kampeni hiyo, kliniki ya afya itafanyika kuanzia Aprili 16-19 ikisaidiwa na Adventist World Radio, 10,000 Toes, na ELIA Wellness.

The original article was published on Adventist Record, the South Pacific Division news site.

Makala Husiani