West-Central Africa Division

Mkutano wa Saba wa Kila Mwaka wa Makambi ya Viziwi Unaonyesha Ushirikishwaji Kaskazini mwa Ghana

Viongozi wa Kanisa la Waadventista na washiriki huanzisha mazingira ya kukaribisha watu wenye ulemavu tofauti, ambayo hupelekea wengi kufanya uamuzi kwa ajili ya Kristo.

Mkutano wa makambi uliwaleta pamoja wawakilishi 93 kutoka makanisa sita ya viziwi katika Eneo la Ashanti [Kwahisani ya: WAD]

Mkutano wa makambi uliwaleta pamoja wawakilishi 93 kutoka makanisa sita ya viziwi katika Eneo la Ashanti [Kwahisani ya: WAD]

Kuanzia Desemba 26–31, 2023, Shule ya Sekondari ya Waadventista huko Agona iliandaa Mkutano wa saba wa kila mwaka wa Makambi ya Viziwi. Tukio hili liliashiria hatua nyingine katika safari ya Konferensi ya Yunioni ya Kaskazini mwa Ghana (NOGH) kuelekea ujumuishi na ukuaji wa kiroho kwa jumuiya yenye ulemavu wa kusikia. Tamaduni hiyo, kuanzia mwaka wa 2014, imekuwa ishara ya umoja katika kanda, inayoakisi kujitolea kwa NOGH kwa utofauti.

Paul T. Danquah, mkurugenzi wa Adventist Possibility Ministries (APM) wa NOGH, na Henry B. Afoakwa, mkurugenzi wa APM wa Konferensi ya Mountain View Ghana, waliongoza tukio hilo kwa usaidizi kutoka kwa Obed Osei-Ajema, wa Konferensi ya Ghana ya Kati. Mkutano wa kambi uliwaleta pamoja wawakilishi 93 kutoka makanisa sita ya viziwi katika Mkoa wa Ashanti, na vikundi kutoka Atimatim, Kwadaso, Bekwai, Sekyedumasai, Atwima Koforidua, na mwenyeji wa kampuni ya Agona.

Mada ya mkutano wa mwaka huu ilikuwa "Upendo Uzaa Upendo." Mzungumzaji mgeni Jallah S. Karbah Sr., mkurugenzi wa APM wa Divisheni ya Afrika Magharibi na Kati, alizingatia mada za upendo na imani katika Kristo, akichota kutoka katika maandiko ya Biblia. Mkutano huo ulionyesha ubatizo wa watu 14, ikiwa ni pamoja na viziwi 11 ambao sio Waadventista, na kukazia hali ya kujumuisha ya tukio hilo. Pia, ulishuhudia ushiriki kutoka kwa jamii yenye uwezo wa kusikia, ikiwa ni pamoja na walimu kutoka shule ya wenyeji, wakichangia kwenye utofauti wa tukio hilo.

Mkutano ulijumuisha ubatizo wa watu 14, ikiwa ni pamoja na washiriki 11 viziwi ambao sio Waadventista
Mkutano ulijumuisha ubatizo wa watu 14, ikiwa ni pamoja na washiriki 11 viziwi ambao sio Waadventista

Programu hiyo ilijumuisha maonyesho ya kwaya ya viziwi na timu ya maigizo, ambao walitumia lugha ya ishara kuwasilisha ujumbe kuhusu upendo na kukubalika. Zaidi ya hayo, tukio hilo lilitoa vipindi vya ushauri kwa wenzi wa ndoa viziwi, kushughulikia changamoto mahususi na kukuza uhusiano imara wa familia.

Mchungaji Henry Brenya Afoakwa, mratibu wa Huduma ya Viziwi kwa NOGH, amekuwa na jukumu muhimu katika kufaulu kwa huduma hii katika yunioni hii. Yunioni na makonferensi mbalimbali yamefanya kazi pamoja kuhamasisha rasilimali, kuhakikisha ushiriki wa walemavu wa kusikia katika mikutano ya Waadventista, ishara ya kuongezeka kwa ushirikishwaji katika jumuiya za kidini.

Kwa vile NOGH inapanga kupanua huduma yake, uungwaji mkono kutoka kwa divisheni, yunioni, na makonferensi ni muhimu. Mkutano wa makambi ya mwaka huu unaonyesha jukumu la imani katika kuziba mapengo ndani ya jamii.

Mkutano unaofuata wa makambi utafanyika Bekwai mnamo 2024, kuendeleza utamaduni wa mikusanyiko hii.

The original version of this story was posted on the West-Central Africa Division website.