Mnamo Mei 8, 2024, gari la mshikamano la ADRA (Shirika la Maendeleo na Misaada la Waadventista) lilifika São Leopoldo, mojawapo ya miji iliyoathiriwa na mafuriko makali huko Rio Grande do Sul, Brazil. Lori hilo limekuwa likisaidia jamii zilizoathiriwa na mvua kubwa tangu Mei 5.
Lori hilo linaweza kuandaa milo 1,500 kwa siku, kuosha na kukausha kilo 105 za nguo kwa kila zamu, na kutoa huduma ya ushauri nasaha kwa jamii. "Lengo letu ni kupitia maeneo yaliyoathirika zaidi ya Rio Grande do Sul, tukileta upendo na huruma kidogo kupitia sahani ya chakula kilicho moto na nguo safi. Ndiyo maana tunaratibu, pamoja na mamlaka za mitaa, vituo vijavyo vya trela," alisisitiza Fábio Salles, mkurugenzi wa ADRA Brazil.
Katika masaa yake 84 ya kwanza ya huduma, lori lilikuwa na usaidizi wy wajitolea 150 na lilisambaza:
Masanduku ya chakula cha mchana 2,350
Kilo 2,900 ya nguo zilizosafishwa
Vikapu 1,2900 vya chakula cha msingi
Vifaa 1,160 vya usafi
Vifaa 1,033 vya kusafisha
Magodoro 140
Nguo 5,775
Jozi za viatu 888
Taulo na vitambaa vya kitanda 2,911
Katika miaka minane iliyopita, lori la mshikamano limegawa milo 178,294 iliyo moto na kuosha tani 191
za nguo, huku likipita katika miji kadhaa ya Brazil, likiitikia
dharura kuu za nchi hiyo.
Kazi ya ADRA
Katika juhudi za kusaidia familia zilizoathiriwa na mvua kubwa huko Rio Grande do Sul, ADRA imeanzisha kampeni ya uchangishaji fedha kupitia mitandao ya kijamii ili kusambaza vocha za matumizi mbalimbali zenye thamani ya takriban reais 1,000 (takriban dola za Marekani 190) kila moja. Vocha hizi zimeundwa ili kusaidia familia kununua bidhaa muhimu kama vile chakula, bidhaa za usafi na za kusafisha, vifaa vya nyumbani, na vifaa vya ujenzi.
ADRA inashirikiana kwa karibu na Sekretarieti ya Maendeleo ya Jamii huko Porto Alegre, mji ulioko Brazil, kusimamia uendeshaji wa makazi ya dharura manne. Vituo hivi, vilivyopo katika Kituo cha Kibinadamu cha FGTAS (Fundação Gaúcha do Trabalho e Ação Social) Vida, Kituo cha Mafunzo ya Michezo ya Jimbo (CETE), na Chuo cha Polisi wa Kijeshi, vina uwezo wa pamoja wa kuhifadhi takriban watu 4,000 jumla.
Mpango huu haupeani tu nafuu ya haraka kwa wale walioathirika na hali mbaya ya hewa bali pia unaunga mkono juhudi za uokoaji zinazoendelea katika eneo hilo.
Kuhusu ADRA
ADRA ni shirika la kimataifa la misaada ya kibinadamu linalofanya kazi katika zaidi ya nchi 120. Kupitia mipango yake, ADRA inalenga kubadilisha maisha na kuimarisha jamii kupitia suluhisho endelevu katika maendeleo ya jamii, usimamizi wa majanga, na kuendeleza haki.
Makala asili ilichapishwa kwenye tovuti ya Kireno ya Divisheni ya Amerika Kusini.