General Conference

Konferensi ya Waadventista wa Utafiti na Matendo ya Familia: Kuimarisha Familia

Konferensi ya 2024 ya Kurejesha Umbizo wa Mwana-Mtu Julai 18-20, 2024 katika Chuo Kikuu cha Andrews

Bango la uelewaji wa familia tofauti. [Imetolewa na Idara ya Huduma za Familia ya Konferensi Kuu]

Bango la uelewaji wa familia tofauti. [Imetolewa na Idara ya Huduma za Familia ya Konferensi Kuu]

Kuanzia tarehe 20 Julai hadi tarehe 22, Kongamano la Waadventista la 2023 kuhusu Utafiti na Mazoezi ya kiFamilia unaoitwa the 2023 Adventist Conference on Family Research and Practice (ACFRP) ulifanyika mutandaoni chini ya mada, "Familia na Afya ya Kihisia: Matumaini, Ponya, Shinda!" Tukio hilo, ambalo lilikaribisha zaidi ya washiriki 2,000 waliosajiliwa kutoka nchi 115, lilikuwa juhudi za ushirikiano kati ya Idara ya Huduma za Familia kwenye Konferensi Kuu, Department of Family Ministries at the General Conference, na Idara ya Uanafunzi katika Elimu ya Maisha Department of Discipleship in Lifespan Educationkatika Seminari ya Theolojia ya Waadventista Wasabato katika Chuo Kikuu cha Andrews University, Shule ya Kazi kwa Jamii katika Chuo Kikuu cha Andrews, na Taasisi ya Kuzuia Uraibu katika Chuo Kikuu cha Andrews. Waliohudhuria walijumuisha washiriki wa kanisa la mtaa, wachungaji, wanafunzi wa seminari, maprofesa, watendaji, na wakurugenzi wa Huduma za Familia kutoka viwango tofauti ndani ya Kanisa la Waadventista Wasabato -Seventh-day Adventist Church

ACFRP ililenga kutoa maarifa muhimu na mikakati ya vitendo ili kukuza ustawi wa kihisia ndani ya familia kufuatia changamoto ambazo hazijawahi kushuhudiwa ndani ya familia katika miaka ya hivi majuzi, ambazo zimezidishwa na janga la COVID-19. Muundo pepe uliwaruhusu washiriki kufikia mawasilisho kwa urahisi wao katika maeneo mbalimbali ya saa na takriban watu 700 walijiunga na tukio katika muda halisi, wakiboresha ubadilishanaji wa mawazo na kuruhusu hali ya jumuiya miongoni mwa waliohudhuria.

Mawasilisho Yaliyotolewa

Wazungumzaji wakuu mashuhuri walicheza jukumu muhimu katika kuunda hotuba ya mkutano huo. Dakt. Kenneth Pargament, msomi mashuhuri katika nyanja ya dini, mambo ya kiroho, na afya, alitoa mwanga kuhusu utafiti wake kuhusu mapambano ya kiroho. Mada yake, "Spiritual Struggles Along the Pathway to Wholeness and Growth," yaani “Mapambano ya Kiroho Katika Njia ya Ukamilifu na Ukuaji,” ilikazia kuenea kwa mapambano ya kiroho kati ya watu wa imani na watu binafsi wa imani mbalimbali.

Wahudhuriaji walipochunguza changamoto na fursa zinazohusiana na maisha ya familia, walikumbuka ujumbe wa mtume Paulo katika 2 Timotheo 3:1-5 kwa maelezo sahihi ya hali ya mchafukoge ya familia katika ulimwengu wa kisasa.

Dk. Willie Oliver, mkurugenzi wa Huduma za Familia katika Koniferensi Kuu, alisema kwamba “Dkt. Morgan Medlock, daktari wa magonjwa ya akili, daktari wa sera ya afya aliyefunzwa Harvard ambaye ni mhariri mkuu wa kitabu Racism and Psychiatry: Contemporary Issues and Interventions, na pia aliyefunzwa katika Seminari ya Theolojia ya Waadventista Wasabato katika Chuo Kikuu cha Andrews, alitoa mfululizo wa sehemu tatu za mawasilisho chini ya rubrika Kutoka Kuvunjika hadi Kufanikiwa (From Breakdown to Breakthrough), ambayo ilikuwa mtazamo wa kibiblia na roho ya unabii wa mkutano huo. Sehemu ya 1 iliitwa Afya ya Akili ya Familia Baada ya COVID-19. Sehemu ya 2 iliitwa Suluhisho Kamili la Mungu, na Sehemu ya 3 ilikuwa Kurejesha Kusudi la Familia. Aliwakumbusha waliohudhuria kwamba familia zetu ‘zinahitaji kutii jumbe za Yohana 15:9, 12, 16 kwa kuelewa kwamba … tunahitaji kujifunza kupendana, na kukumbuka kwamba tumechaguliwa na Mungu kuwa sehemu ya familia Yake, kwa hiyo hatupo peke yetu kamwe.’”

Mkutano huo ulitoa fursa za kushiriki kikamilifu kupitia mijadala ya paneli na vipindi vifupi. Waliohudhuria walishiriki katika vipindi vya Maswali na Majibu na wazungumzaji wakuu ili kutafakari kwa kina dhana zilizowasilishwa. Vipindi vifupi vilivyotolewa na wasomi na wanafunzi waliohitimu vilishughulikia maswala muhimu kama vile athari ya kufungiwa kwa waalio na ugonjwa wa kiakili kwa familia, uzazi kwa ujasiri, jukumu la wazazi, athari za mitandao ya kijamii, ndoa, na ponografia kwenye afya ya kiakili, na uhusiano kati ya kiwewe cha utotoni, na ukomavu wa imani, miongoni mwa mengine.

Matokeo ya Ubunifu

Miongoni mwa matokeo ya kibunifu yaliyowasilishwa, mjadala wa Dk. Pargament juu ya "Ninawezaje Kuishi na Mimi Mwenyewe? Nikiwasaidia Watu Katika Nyakati za Mapambano ya Maadili" ulijitokeza. Aliangazia uhusiano uliopo kati ya matatizo ya kisaikolojia, kama vile wasiwasi, mfadhaiko, uraibu, kuumia kiadili, ukiukaji wa maadili, na mapambano ya kimaadili.

Mkutano huo pia ulijadili athari za changamoto za kisasa, haswa teknolojia na mitandao ya kijamii, katika mienendo ya familia. Waliohudhuria walijifunza kwamba janga jipya la upweke na shida ya afya ya akili ya vijana inahusiana kwa karibu na matumizi ya kila mara ya media na sehemu kubwa ya idadi ya vijana.

Tukio lilipohitimishwa, waandaaji waliwapa changamoto washiriki kutumia matokeo ya utafiti na dhana zilizojadiliwa katika maisha yao ya nyumbani ili kuimarisha afya yao ya kihisia na ya familia zao. Dk. Medlock alisisitiza umuhimu wa kuishi kwa agano la upendo usio na masharti, neema, uwezeshaji, na urafiki ndani ya familia.

Tukiangalia siku zijazo, Kongamano la Waadventista la 2024 kuhusu Utafiti na Mazoezi ya Familia linatazamiwa kufanyika kuanzia Julai 18-20, 2024, likiwa na mada, “Kuelewa Familia Mbalimbali.” Mkutano huo utarudi kwa muundo wa kibinafsi katika Chapel ya Seminari - Seminary Chapel kwenye kampasi ya Chuo Kikuu cha Andrews. Waandaaji wanatarajia kujumuisha mbinu mseto ili kuruhusu washiriki wa kimataifa kushiriki hata kama hawawezi kuhudhuria ana kwa ana.

Kongamano la mtandaoni la ACFRP la 2023 limefaulu, likihimiza familia na watendaji kote ulimwenguni kukuza ustawi wa kihisia na kuimarisha jumuiya zao. Kwa kukuza ushirikiano na kushiriki utafiti wa kibunifu, ACFRP inaendelea kuwa mwanga wa matumaini na usaidizi kwa familia katika enzi ya kisasa.

To watch the general session presentations and seminars of the 2023 ACFRP, click here.