Inter-European Division

Kanisa la Waadventista huko Italia Latoa Kitita cha €13,000 kwa Waathirika wa Mafuriko

Mashirika mengi, ikiwa ni pamoja na ADRA, yalishirikiana pamoja ili kutoa misaada baada ya maafa ya katikati ya mwezi Mei

Picha kwa hisani ya: Divisheni ya Inter-European

Picha kwa hisani ya: Divisheni ya Inter-European

Jumamosi, Oktoba 28, 2023, katika kanisa la Waadventista huko Cesena, Italia, waliohudhuria walijionea kilele cha Tamasha la 22 la Mshikamano, lililofanyika awali wikendi ya Septemba 2–3 na 9–10 ili kuchangisha fedha kwa ajili ya waathiriwa wa mafuriko ya Cesena.

Mkutano huo ulijumuisha kukabidhi mapato kwa Il Barco, ikiwakilishwa na mratibu wake, Susanna Ricci. Il Barco ni mukusanyiko wa mashirika manane katika eneo hilo (ikiwa ni pamoja na Shirika la Maendeleo na Misaada la Waadventista [ADRA]) ambayo, yakiwa na uzoefu mkubwa katika uwanja wa mshikamano, yaliungana mara moja na kuchukua hatua kusaidia familia nyingi zilizoathiriwa kwa kiasi kikubwa na mafuriko ambayo yalikumba sehemu kubwa ya eneo la Emilia-Romagna katikati ya mwezi wa Mei.

Kabla ya hafla ya makabidhiano, waliohudhuria walisikiliza uzoefu wa Marco Raffaele, mmoja wa watu wengi walioathiriwa moja kwa moja na mafuriko. Alisimulia nyakati ngumu alizopitia na kuwashukuru kwa moyo wote “mud angels” waliomsaidia yeye na jiji zima.

Baada ya wakati huu wa mguso, hundi ya €13,000 (takriban US$14,250) ilikabidhiwa kwa Il Barco. ADRA Italia iliingilia kati ili kufanikisha hili, ikitoa €5,000 (takriban US$5,480) kama sehemu ya fedha zilizokusanywa wakati wa awamu ya dharura. The 8xmille ya Kanisa la Waadventista pia iliunga mkono mpango huo.

Kwa shukrani na tafakari, viongozi wanne pia walishiriki katika hafla hiyo: Carmelina Labruzzo, diwani wa huduma kwa watu na familia wa Manispaa ya Cesena; Giovanni Benini, mratibu wa Tamasha la Mshikamano; Roberto Iannò, mchungaji wa kanisa la Waadventista huko Cesena; na Giuseppe Cupertino, mkurugenzi wa Osa, ambaye anasimamia 8xmille iliyoteuliwa kwa ajili ya Kanisa la Waadventista.

The original version of this story was posted on the Inter-European Division website.