Kanisa la Waadventista huko Fiji Lajitolea Kuunda Nafasi Zinazoweza Kufikiwa

South Pacific Division

Kanisa la Waadventista huko Fiji Lajitolea Kuunda Nafasi Zinazoweza Kufikiwa

Ukarabati wa hivi majuzi unaangazia kuongezeka kwa juhudi za kanisa kukuza mazingira ya kujumuishwa kwa wale walio na ulemavu

Ofisi ya Misheni ya Unioni ya Pasifiki na Viunga vyake huko Tamavua, Suva, Fiji, sasa ni nafasi ya rafiki kwa watu wenye ulemavu, yaani disability-friendly space, kutokana na kazi kubwa ya kurekebisha iliyoratibiwa na ADRA (Shirika la Maendeleo na Misaada la Waadventista) Fiji. Hafla rasmi ya makabidhiano ya vifaa vipya vya ushirikishwaji au ufikiaji ilifanyika Septemba 26, 2023 katika makao makuu ya TPUM.

Mpango huu ni sehemu ya mradi mkubwa wa Makanisa ya Fiji ambayo ni Disaster Ready, unaofadhiliwa na Divisheni ya Pasifiki ya Kusini ya Waadventista Wasabato kupitia ADRA Pasifiki ya Kusini.

Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu la Fiji (FDPF) lilijiunga na maadhimisho hayo, ambayo yaliashiria hatua kubwa mbele katika kuhakikisha ushirikishwaji na ufikiaji kwa wanachama wote wa jumuiya ya FDPF.

Jay Nasilasila, mratibu wa programu ya FDPF ya Kupunguza Hatari za Maafa (DRR), alihutubia mkutano huo kwa shauku, akisisitiza umuhimu wa hatua hii muhimu kwa jumuiya ya FDPF. "Tunaamini kwamba kila mtu, bila kujali uwezo wake wa kimwili, anastahili fursa sawa na upatikanaji wa nafasi za umma. Ni kanuni ya msingi ya usawa ambayo tunaiheshimu sana. Leo, tunachukua hatua madhubuti kugeuza kanuni hii kuwa ukweli,” alisema.

Nasilasila alielezea zaidi muundo wa kina wa vifaa, akionyesha urahisi na faraja kwa watu binafsi wenye mahitaji mbalimbali. "Tumefanya kazi kwa karibu na wataalam na jumuiya ya walemavu ili kuhakikisha kuwa vifaa hivi vinafikia viwango vya juu vya ufikivu," aliongeza.

Nasilasila alisisitiza kwamba jitihada hii haikuwa tu wajibu wa kisheria bali ni ushahidi wa kujitolea kwa kanisa kuunda jamii iliyohusisha kila mmoja zaidi. "Tunaamini kwa dhati kwamba ufikiaji ni jukumu la pamoja, na kwa kanisa kuwa mfano huu, tunatumai utawatia moyo wengine kufanya vivyo hivyo."

Kama sehemu ya Mradi wa Makanisa ya Fiji abayo yako Tayari kwa Majanga yaani Disaster Ready, jumla ya mali (majengo) saba ya kanisa za Misheni ya Fiji yamefanyiwa marekebisho ili kujumuisha zaidi. Mpango huu unaongeza mafunzo ya kitaifa ya kudhibiti hatari za maafa katika makanisa ya mtaa, kuwapa washiriki maarifa ya kujiandaa kwa majanga yeyote.

Mchungaji Maveni Kaunfononga, rais wa TPUM, alitoa shukrani zake kwa ADRA Fiji kwa kuanzisha mradi huo. Alisisitiza kuwa, jitihada hii ni kutambua upendo na utunzaji wa kanisa kwa waumini wake wenye ulemavu. "Katika ufalme wa Mungu, kuna upendo, na upendo huo lazima ufanyike tukiwa hapa duniani, hivyo mradi huu ni kielelezo cha upendo wa Mungu kwetu," alisema Mchungaji Kaufononga.

Ana Alburqueque, mshauri wa ADRA Pasifiki ya Kusini, alisisitiza kujitolea kwa ADRA kusaidia makanisa katika Pasifiki kuwa tayari kwa majanga (Disaster Ready), kutokana na uwezekano wa eneo hilo kukabiliwa na majanga. Alibainisha kuwa timu hiyo inafanya kazi kwa bidii kusaidia nchi tano za kikanda.

The original version of this story was posted on the Adventist Record website.