Siku ya pili ya Mkutano wa Majira ya Kuchipua wa 2025 wa Konferensi Kuu (GC) ilihitimishwa na Kamati ya Utendaji kupiga kura kuidhinisha miongozo ya Vikundi vya Nyumbani.
Mazungumzo kuhusu Vikundi vya Nyumbani yalianza katika Baraza la Kila Mwaka la 2024. Kisha iliamuliwa kupeleka neno hilo kwa Kamati ya Mwongozo wa Kanisa ili kuandaa miongozo rasmi kwa vikundi hivyo.
Gerson Santos, katibu msaidizi wa GC, aliwasilisha miongozo mipya ya Mwongozo wa Kanisa kuhusu Vikundi vya Nyumbani, akibainisha kuwa ingawa maneno 'Vikundi vya Nyumbani' na 'Makanisa ya Nyumbani' yatatumika kwa kubadilishana ndani ya mwongozo, 'Vikundi vya Nyumbani' litakuwa neno linalopendelewa.
Santos alieleza kuwa miongozo hiyo imelenga kuwafikia watu wengi iwezekanavyo na tangazo la Kanisa la Waadventista wa Sabato la Ujumbe wa Malaika Watatu, akitambua kuwa mikusanyiko ya kanisa inaweza kutofautiana kulingana na muktadha wa kanda.
“Katika nyakati za Agano Jipya, Wakristo wa mapema walikusanyika majumbani, na leo mbinu ya uhusiano ya kikundi cha nyumbani inaweza kuunda wanafunzi katika maeneo ambapo ibada ya wazi imezuiliwa,” alisema Santos.
Richard McEdward, rais wa Yunioni ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, alithibitisha uamuzi huo, akisisitiza umuhimu wa Vikundi vya Nyumbani katika eneo hilo.
Majadiliano kati ya wajumbe yalichochea uthibitisho kwamba Mwongozo wa Kanisa la Waadventista wa Sabato unafanya kazi ya kutofautisha Vikundi vya Nyumbani na vikundi vingin vidogo. Kulingana na mwongozo huo, kikundi kidogo ni kikundi cha waumini wanaokutana wakati wa wiki, lakini huja kanisani kwa ibada. Kikundi cha Nyumbani hukutana katika eneo lililokubaliwa na washiriki ili kufanya ibada.
Kamati Kuu ya Utendaji ilipiga kura 132-1 kuunga mkono miongozo hiyo.
Jiunge na Chaneli ya ANN ya WhatsApp kwa habari za hivi punde za Waadventista.