Siku moja baada ya helikopta hiyo kutoweka, timu za upekuzi ziligundua jozi ya viatu baharini, vya Janelle Alder, muuguzi wa medivac ndani ya helikopta iliyopotea.
Ndege ya aina ya helikopta ya kiadventista ya PAMAS (Huduma za Usafiri wa Anga za Waadventista wa Ufilipino) imekosekana kwa muda wa siku tano na utafutaji unaendelea ukisaidiwa na makundi mengi na watu wengi. Utafutaji wa ndege hio umekuwa wa hali ya juu, ukienezwa kwa maeneo yaliyokisiwa kuw ya mkosi na maeneo ya karibu.
Kampuni ya uokoaji ya Philipi iitwayo (The Philippines Aviation Rescue Coordination Center, PARCC) inafanya kazi kwa karibu na ile ya Kota Kinabalu Aviation Rescue Coordination Center (KKARC) kwa kutuma mashua tano na ndege tatu, zikiwemo zile za C130, kule malaysia kwa utafiti wa maji na hewa. Serekali ya nchi ya Malaysia imetoa usaidizi wao ambao umepokelewa vizuri na kampuni ya PAMAS.
Watafiti wa kujitolea wa miale ya jua na vifaa vyao walifika Puerto Princesa, Philipi. Watafiti hao walisafirishwa na kampuni ya jeshi ya anga la Philipi hadi PAMAS hangar, kisha kusafirishwa na ndege mbili za PAMAS kwenda Candarman, kiziwa karibu na eneo kulikokuwa tafiti za maji. Watafiti hao walikutana na wanajeshi wa hewani wa Philipi ili kupanga usafiri wao hadi maeneo yaliyokisiwa.
Siku iliyofuata siku ya helikopta kupotea, Shirika la Municipal Disaster Risk Reduction and Management office (MDRRMO) ilivigundua viatu katika bahari ambavyo waliwapokeza maafisa wa PAMAS. Watu wengi walisadiki kuwa vilikuwa vya Janelle Alder, mwuguzi ambaye aliabiri helikopta iliyopotea.
Juhudi za waliohusika zimeweza kupigiwa mfano, na hata mafuta ya ndege yako njiani. Lau Dagum, Rafiki aliyejipanga kuja kwa wakati wa mwisho na vifaa muhimu, alishukuriwa pia. Dagum hufanya na Antipara Explorations, wanaojihusisha na utafutaji na kupima hali kule kwenye maji, na anafanya shahada yake ya uzamivu katika masomo ya bahari.
Toleo la asili la hadithi hii lilichapishwa kwenye tovuti ya Idara ya Kusini mwa Asia-Pasifiki.
The original version of this story was posted on the Southern Asia-Pacific Division website.