Idara ya Amerika Kaskazini Inajiunga na Mpango wa Mradi wa "Pambano Kuu" wa 2023-2024

[Picha: Pacific Press Publishing Association].

North American Division

Idara ya Amerika Kaskazini Inajiunga na Mpango wa Mradi wa "Pambano Kuu" wa 2023-2024

Mpango huo unalenga kusambaza nakala bilioni 1 za Pambano Kuu ya Ellen White duniani kote.

Wakati wa mkutano wa watu wa kawaida wajulikanao kama Adventist Laymen’s services and Industries (ASI) Agosti, 2021, Ted Wilson, Rais wa Kanisa ulimwenguni alitangaza mapango wa kusambaza vitabu milioni moja vya Pambano kuu vilivyoandikwa na Ellen White ulimwenguni. Kitabu hicho ni nyenzo kuu katika kueneza injili na kimekuwa cha manufaa sana katika mazungumzo ya waadventista wengi ulimwenguni. Trouble on the Blue Planet- Kitabu kinachoelekezwa kwa vijana

Mpangilio huu unawashawishi waadventista kukisoma na kuusambaza ujumbe wa kitabu hiki kilicho mjowapo ya vitabu vitano vya msururu wa pambano la vizazi. Pambano kuu ni mtazamo mkuu wa historia ya kanisa kutoka kwa msingi wa kibibilia na mwisho ushindi juu ya shetani.

“Neno lilioandikwa n msingi wa neno linalohubiriwa,” alisema Carl McRoy msimamizi wa idara ya vitabu kule Amerika kusini. “Inawaandaa watu kwa ajili ya mahubiri ya mdomo ya injili na kufanya imara hoja zitolewazwo kutoka kwenye matabau na hata vyombo vya habari, mara nyingi hujibu maswali ambayo huibuka kutoka kwa kusikiza mahubiri ama uchambuzi wa Bibilia.

Wakati wa hatua za kwanza za 2023, Divisheni ya Amerika kusini inawahimiza washiriki kujiunga. Katika hatua za hapo awali, mtazamo ulikuwa katika usambazaji wa vitabu, aidha kupitia kuzunguka mlango hata mlango au kupitia kwa barua pepe. Mipango hii hufanya vizuri katika maeneo mengine, ilhali katika maeneo mengine, njia ya moja kwa moja inaweza tia fora.

Washiriki wanaotaka kujiunga wanaweza kusambaza vitabu kwa Rafiki wao, familia na jamii kupitia njia nyingi kama vile mahojiano ya moja kwa moja, utimizi wa mtandao na hata katika makundi.

SOMA KWANZA

Hata ingawa Pambano kuu n mojawapo ya kitabu tajika kilichoandikwa na mojawapo ya waanzilishi wa kanisa, baadhi ya washiriki huenda hawajapata nafasi ya kukisoma. “Napendezwa na mpangilio unaozuka wa kuwapa watu vitabu vya “Tumaini la Vizazi” na “Pambano Kuu” ikiwemo watu wa familia, Rafiki na wenzetu,” alisema G. Alexander Bryant, Rais wa NAD. “Tunamsihi kila mmoja kote katika Divisheni kusoma au kusoma tena kitabu hiki cha kupendeza kwa wakati wetu.” Yeyote anaweza kukipokea katika mtandao kupitia WWW. TheGreatControversy.org. Unaweza kipata kitabu kizima kwenye mtandao, au ukasikiza sauti za kitabu zilizonakiliwa, au ukapakua nakala au EPUB. Kwa wale wanaopendezwa na kitabu kilichochapishwa, taasisi ya uchapishaji ya Pacific press Publishing Association inatoa chapisho Zaidi ya dazani ya vitabu vya White Estate katika WWW. AdventistBookCenter.com/GreatControversy. Pata chapisho la angalau kila mmoja na katika kila lugha.

Pambano kuu ni kitabu kizuri kwa makundi madogo na uchambuzi wa Bibilia. Maelekezo ya mafunzo sasa yanaweza patikana kusaidia makundi madogo na uchambuzi wa kibinafsi.

Jiunge na Mpangilio

Hatua nyingine, ni ya kujumuishwa, na kuna njia nyingi za kufanya hivo. Watu binafsi wanaweza fanya kupitia kwa mzunguko wa ushawishi wao- marafiki, familia, wenzao- kuona upokezi na kuwapa vitabu. Kusanyiko za kanisa wanaweza kufuata mipangilio mikubwa za kusambaza vitabu vingi katika sherehe na mikutano katika jamii. Kanisa nyingine zinabania kutumia mbinu nyingi pamoja, wakianza kusambaza Tumaini la vizazi au Hatua kuelekea kwa yesu. “Wakati mtulivu na kitabuu na Roho mtakatifu n mpango mzuri wa kueneza Bibilia kwa watu ambao ni wagumu kuwafikia,” alisema McRoy. Zaidi watu husahau ila karatasi hukumbuka.

Kanisa kuu ulimwenguni limeanzisha mtandao wa mpango huo: WWW. GreatControversyProject.org. Mtandao huu una pendekezo nzuri la kuliwasilisha katika kikao cha Baraza la kanisa, ujumbe jinsi ya kuomba vitabu vingi kwa pamoja, matini ya kuhimiza na mpangilio wa kusoma na kujifunza kwa kitabu.

Machapizo ya Uchapishaji wa Pacific

Baadhi ya chapisho za taasisi hii ya uchapisho ni mfano tafsiri za Kihispania, Kifaransa, kireno na hata lugha nyingenezo zitaongezwa mwaka huu. Chapisho Zaidi ni kwa mfano

TGCP – Kitabu kizima, katika karatasi kwa bei nafuu, bei nzuri kwa vitabu vingi, utmiaji wa msimbo wa zip vikiwemo katika lugha ya Kiingereza, kihispania, kifaransa na karibuni kireno.

ASI 2022- Kitabu kizima, katika karatasi kwa bei nafuu, bei nzuri kwa wanaotaka kusambaza kibinafsi

Christian Home Library- Kitabu kizima, Katika karatasi

Leather Edition – Kitabu kizima, katika karatasi

Standard Paperback- Kitabu kizima, katika karatasi

Gift Edition – Kitabu kizima, Katika karatasi

New King James Edition – Kitabu kizima chenye marejeleo ya NKJV

Illustrated Edition- Kiatbu kizima na maonyesho

Darkness Before Dawn- Baadhi ya maeneleo ya kitabu

The Great Hope- Baadhi ya maeneo ya kitabu yaliyofupishwa

Love Under Fire – Ufupisho wa uchapisho katika lugha husika

Michael Asks Why – Kitabu cha ujuzi kwa Watoto

War of the Invisibles- Kunongeza kwa wanarika kupitia kwa macho ya malaika