Loma Linda University Health (LLUH) kimetambuliwa na Newsweek kwa ushirikiano na Statista kuwa miongoni mwa Hospitali Bora Maalum za Marekani mwaka wa 2024 kwa ajili ya magonjwa ya moyo, utunzaji wa neva, na mifupa na viungo. Hospitali ya Watoto ya Chuo Kikuu cha Loma Linda (LLUCH) pia ilitambuliwa miongoni mwa Hospitali Bora za Watoto za Marekani mwaka wa 2024 kwa ajili ya utunzaji wa watoto wachanga.
Utambuzi huo unatokana na uchunguzi wa kitaifa wa watoa huduma za afya na wasimamizi, viashirio muhimu vya utendaji kazi, tafiti za uzoefu wa wagonjwa na na matokeo yaliyoripotiwa na wagonjwa kupitia Statista.
"Utambuzi huu unasisitiza utaalamu wetu na utunzaji wa huruma unaopatikana katika kila timu maalum," alisema Trevor Wright, MHA, FACHE, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali za Loma Linda University Health. "Wagonjwa wanaweza kuhakikishiwa kuwa wanapokea huduma bora zaidi hapa katika eneo lao la nyumbani," aliongeza.
LLUH hutoa utunzaji maalum kwa eneo kubwa katika kaunti nne, inayojumuisha takriban robo moja ya jimbo la California.
Utunzaji wa moyo (cardiac care) wa LLUH ndio ulio wa hali ya juu zaidi katika kanda, pamoja na kituo chake cha utunzaji wa hali ya juu na timu za wataalam wa taaluma nyingi. Utunzaji wake wa neza ( neurological care) ni pamoja na kituo cha kifafa, kituo cha kumbukumbu, kituo cha kiharusi, na utunzaji wa hali ya juu wa neuromuscular. Utunzaji wa mifupa (orthopaedic care ) wa LLUH ni pamoja na dawa ya michezo, uingizwaji wa viungo, na utunzaji wa uti wa mgongo.
NICU ya Level 4 ya vitanda 84 huko LLUCH inatibu watoto wachanga wanaohitaji huduma ngumu zaidi, ikiwa ni pamoja na watoto wadogo waliozaliwa na uzito wa chini ya paundi 2.2. Mbali na madaktari wa watoto wachanga, watoto wa NICU wanasaidiwa na timu nzima ya wataalam katika hospitali nzima na Banda la Wazazi la San Manuel.
Makala asili ilichapishwa kwenye tovuti ya Loma Linda University Health