Hafla ya uzinduzi ilifanyika katika eneo ambalo kituo kipya cha habari kitajengwa, huko Kinshasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Shirika la Hope Channel International (HCI) hivi majuzi lilizindua mpango mpya wa ujumbe wa vyombo vya habari unaolenga Kinshasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mpango huu, unaojumuisha ujenzi wa kituo cha kisasa cha vyombo vya habari, utawafikia zaidi ya watu milioni 18 katika jiji hilo ambalo lina idadi kubwa ya watu Kusini mwa Jangwa la Sahara. Ni ushirikiano kati ya HCI, Adventist World Radio (AWR), Divisheni ya Afrika ya Mashariki na Kati (ECD), Unioni ya Kongo Magharibi, na Konferensi Kuu ya Waadventista Wasabato.
Mnamo Oktoba 21, sherehe ya uzinduzi ilifanyika katika tovuti ambapo kituo kipya cha habari kitajengwa. Viongozi kutoka Hope Channel ya Kimataifa, Redio ya Dunia ya Waadventista, Divisheni ya Afrika ya Mashariki na Kati, na Unioni ya Kongo Magharibi walishiriki katika sherehe hiyo huku maelfu ya washiriki kutoka makanisa ya mitaani ya Kinshasa wakihudhuria.
Rais wa ECD Blasious Ruguri, alisema, "Hiki kitakuwa kituo kikuu cha utume kwa programu za lugha ya Kifaransa, kutumia vyombo vya habari kufikia mamilioni ya watu huko Kinshasa na kwingineko, kwa ulimwengu wote unaozungumza Kifaransa." Musa Mitekaro na Yohannes Olana, katibu mtendaji wa ECD na mweka hazina mtawalia, waliandamana na Mchungaji Ruguri wakati wa hafla hii. "Hope Channel itatangaza jumbe za matumaini katika lugha za Kifaransa na Kilingala kutoka kituo hiki cha vyombo vya habari na vipindi vya imani, afya, na maisha bora kwa familia na jamii," Mchungaji Ruguri alisema.
Wakati huo huo, Makamu wa Rais wa Fedha wa AWR Delbert Pearman alisema, "Hii ni mara ya kwanza AWR na HCI zinashirikiana katika mpango mkubwa wa kuanzisha kituo kikuu cha media huko Kinshasa. AWR inataka kituo hiki cha vyombo vya habari kiwe kitovu kikuu cha kimataifa cha kutengeneza vipindi vya Kifaransa." Rais wa Unioni ya Kongo Magharibi Lamec Barishinga alielezea kushukuru kwa kituo cha habari kilichopo Kinshasa na kuahidi uungwaji mkono kutoka unioni hiyo na kutoka kwa swahiriki katika kutumia vyombo vya habari kama chombo cha juhudi zao za uinjilisti.
Pearman na Makamu wa Rais wa Feha wa HCI Gideon Mutero walishiriki ujumbe kutoka kwa AWR na Hope Channel mtawalia na Mchungaji Ruguri akatoa maombi ya kuwekwa wakfu katika tovuti hiyo. Hope Channel International inafikia mipaka mipya ya dhamira na kwa usaidizi wako, athari ya kuzidisha ya vyombo vya habari itapanuliwa kufikia mamilioni ya watu.
Kuhusu Hope Channel
Hope Channel International Inc. (HCI) ni mtandao wa vyombo vya habari vya Kikristo duniani kote ambao hutoa programu kuhusu maisha ya Kikristo inayozingatia kikamilifu imani, afya, mahusiano na jumuiya. Hope Channel ilianza kutangaza Amerika Kaskazini mwaka wa 2003. Leo, Hope Channel ni mtandao wa kimataifa wenye zaidi ya chaneli 80 zinazotangaza katika zaidi ya lugha 100.
This story was provided by Hope Channel Internacional