Southern Asia-Pacific Division

AWR Yafanya Mafunzo ya Vituo vya Lugha 100 huko Bangkok

Kanisa la Waadventista kwa sasa linatoa huduma kwa zaidi ya lugha 443 duniani kote.

Viongozi wa mawasiliano, watengenezaji wa maudhui ya redio, na watayarishaji walikusanyika Bangkok, Thailand kuanzisha mpango wa Asia na Pasifiki kwa Ajili ya Redio ya Waadventista Duniani (Adventist World Radio, AWR). Lengo ni kuandaa maudhui katika lugha 100, kwa nia ya kuwafikia wasikilizaji mbalimbali duniani kote kwa lugha zao za asili.

Viongozi wa mawasiliano, watengenezaji wa maudhui ya redio, na watayarishaji walikusanyika Bangkok, Thailand kuanzisha mpango wa Asia na Pasifiki kwa Ajili ya Redio ya Waadventista Duniani (Adventist World Radio, AWR). Lengo ni kuandaa maudhui katika lugha 100, kwa nia ya kuwafikia wasikilizaji mbalimbali duniani kote kwa lugha zao za asili.

[Picha: Idara ya Mawasiliano ya Divisheni ya Kusini mwa Asia na Pasifiki]

Wakati kongamano la Mkutano wa Teknolojia wa Waadventista ( Adventist Technology Summit, ATS) na la Mtandao wa Ulimwengu wa Interneti wa Waadventista(Global Adventist Internet Network, GAiN) lilipomalizika huko Chiang Mai, Thailand, Redio ya Waadventista Duniani ( Adventist World Radio, AWR), iliitikia kwa haraka kwa kuanzisha mafunzo yao ya kwanza ya vituo vya lugha 100 huko Bangkok. Tarehe 16 Julai, 2024, zaidi ya mameneja 100 wa vituo, viongozi wa mawasiliano, na watengenezaji wa maudhui walikusanyika katika Hoteli ya Hilton Sukhumvit katika mji mkuu wa biashara wa Thailand, nchi kubwa zaidi ya Wabudha Kusini-Mashariki mwa Asia.

Mafunzo haya ya kwanza kwa lugha 100 yanaitikia wito wa kushiriki injili kwa lugha mbalimbali duniani kote, hasa ndani ya dirisha la 10/40. Utafiti wa hivi karibuni unaonyesha kuwa kuna zaidi ya lugha na lahaja 7,100 duniani kote. Kanisa la Waadventista kwa sasa linawafikia watu kupitia zaidi ya machapisho 270, zaidi ya njia 280 za matangazo, na kwa kuzungumza kwa lugha 443. Takwimu hizi zinaonyesha changamoto kubwa kwa kanisa, zikisisitiza haja ya uelewa wa wazi na hisia ya haraka katika katika kuendeleza kazi ya kanisa katika eneo hili.

Robert Dulay, mkurugenzi wa AWR wa Asia na Pasifiki, alifungua mafunzo kwa kusisitiza nafasi muhimu ambayo kila mshiriki wa kanisa analo katika kutangaza ujumbe wa matumaini kwa kizazi hiki. “Bado kuna mengi ya kufanya, na kila mmoja wetu hapa lazima ashiriki kwa uwezo ambao Mungu ametukabidhi ili kushiriki ujumbe Wake na kila kabila, jamaa, lugha, na watu,” alisema Dulay.

“Kufanya Neno la Mungu lipatikane katika maelfu ya lugha duniani kote ni changamoto kubwa, lakini kupitia ushirikiano, kutegemea mwongozo wa Mungu, na kujitolea kwa misheni Yake, juhudi zetu zitazaa matunda,” aliongeza.

Wakati wa mafunzo ya siku mbili, washiriki walipata mafunzo ya kina kuhusu maendeleo ya vipindi vya redio na maelekezo ya kiufundi. Wataalamu kadhaa katika uwanja huu walitoa maarifa muhimu kuhusu matumizi na zana za hivi majuzi kwa ushirikiano na uundaji wa maudhui ya redio.

Neville Neveling, msaidizi wa rais wa AWR, pamoja na timu yake ya wataalamu wa kiufundi na watengenezaji wa maudhui, walihudhuria mkutano huo ili kuwawezesha watengenezaji wa maudhui Waadventista kutengeneza maudhui kwa lugha maalum, wakilenga hadhira maalum.

Mafunzo hayo yalihitimishwa na ahadi mpya kutoka kwa washiriki wote kuendeleza misheni ya Redio ya Waadventista Duniani. Wakiwa na ujuzi mpya na maono ya pamoja, washiriki sasa wako tayari kutengeneza maudhui yenye athari ambayo yatawiana na hadhira mbalimbali duniani kote.

Makala asili ilichapishwa kwenye tovuti ya Divisheni ya Kusini mwa Asia na Pasifiki.