ADRA Yakabiliana na Kimbunga huko Vanuatu

South Pacific Division

ADRA Yakabiliana na Kimbunga huko Vanuatu

Vanuatu ilitangaza hali ya hatari baada ya kundi la nne la Kimbunga Kelvin kukumba eneo hilo mnamo Machi 3, 2023.

Vanuatuimetangaza hali ya hatari huku aina 4 ya Kimbunga Kevin ikikumba kisiwa hicho mnamo Ijumaa ,Machi 3,2023, na kuharibu nyumba na kuwaacha wengi wakihitaji makazi.Nchi hiyo tayari ilikuwa imekumbwa na hali mbaya ya hewa siku mbili zilizopita baada ya Kimbunga Judy kupiga Port Vila mnamo Machi 1.

Miti mingi ya matunda iliangamizwa , na kuathiri familia zinazotegemea mavuno kwa chakula na mapato.Mafuriko makubwa pia yameathiri jamii za Tanna, na wengi wanasalia bila nguvu.

(Picha: Rekodi ya Waadventista)
(Picha: Rekodi ya Waadventista)

Tanna, na visiwa vingine vilivyo kusini mwa Vanuatu havina mawasiliano ya simu , kumaanisha kuwa jamii nyingi zimeshindwa kuwasiliana na zingine.

Shirika la Maendeleo na Usaidizi la Waadventista ADRA liko majumbani Vanuatu likijibu.Shirika la misaada ya kibinadamu lilifungua vituo viwili vya uokoaji-kimoja huko Santo na kingine huko Port Vila-kutoa makazi wakati wa kimbunga . Kituo hicho katika Port Vila ,mji mkuu wa taifa hilo ,kinaendelea kuwa wazi,na kutoa makazi kwa watu ambao wamepoteza makazi yao, pamoja na huduma za chakula na ushauri.

(Picha: Rekodi ya Waadventista)
(Picha: Rekodi ya Waadventista)

Timu ya ADRA mashinani inashughulikia kutafiti mahitaji ya jamii zilizoathiriwa ili kubaini jinsi bora ya kujibu.Mchungaji Thomas Belden , meneja wa mradi wa ADRA ,Vanuatu,ambaye anaendesha mradi wa afya huko Efate ,alikuwa mmoja wa kwanza kufanya tathmini ya mahitaji ya haraka ya jumuiya yake ya ndani.

Misheni ya Vanuatu inafanya kazi kwa karibu na ADRA ili kutoa usaidizi ,na kituo cha operesheni za dharura cha ADRA kimeanzishwa katika ofisi ya misheni.

Mchungaji Thomas (kushoto) akiwa na jumuiya yake ya mtaani. ADRA kwa sasa inaendesha mradi wa kufikia afya unaosimamiwa na Mchungaji Thomas. (Picha: Rekodi ya Waadventista)
Mchungaji Thomas (kushoto) akiwa na jumuiya yake ya mtaani. ADRA kwa sasa inaendesha mradi wa kufikia afya unaosimamiwa na Mchungaji Thomas. (Picha: Rekodi ya Waadventista)

Timu ya ADRA ya nchini Vanuatu inashirikiana na timu ya kukabiliana na kanda na wanachama kutoka ADRA Pasifiki ya kusini ,ADRA New zealand , na ADRA Australia.

‘’Timu yetu ya ndani uwanjani imekuwa ya kushangaza;wametumia wikendi hii iliyopita kuweka jibu la dharura ili kusaidia familia wanapohitaji Zaidi,’’anashiriki Anna Cherry,mwanachama wa timu ya mwitikio wa kikanda na meneja wa programu wa ADRA New Zealand.

Ili kusaidia kazi ya kukabiliana na maafa ya ADRA tafadhani tembelea ˸

www.adra.org.au/disaster[Australia]

www.adra.org.nz/help[New Zealand

Toleo la asili la hadithi hii ilichapishwa kwenye tovuti ya habari ya idara ya Pasifiki kusini,Rekodi ya Waadventista.