General Conference

ADRA Inaendelea Kutoa Msaada nchini Myanmar na Bangladesh

ADRA imekuwa ushukani nchini Myanmar na Bangladesh kufuatia athari za Kimbunga cha Mocha, kilicholikumba eneo hilo mapema mwaka wa 2023.

United States

[Picha: ADRA]

[Picha: ADRA]

Shirika la Maendeleo na Misaada la Waadventista (ADRA) limekuwa likifanya kazi nchini Myanmar na Bangladesh kufuatia athari za Kimbunga Mocha, kilichopiga eneo hilo mapema mwaka huu Mei 14. Dhoruba hiyo iliathiri karibu watu milioni 3.4. Mawimbi hayo makubwa yasababisha mafuriko maeneo ya pwani na kwa jamii nyingi, na kusababisha mvua kubwa, upepo mkali na kusababisha maporomoko ya ardhi.

Kulingana na mamlaka ya kitaifa ya kudhibiti majanga, watu wasiopungua 148 waliuawa na zaidi ya 700 kujeruhiwa. Zaidi ya watu 200,000 walikuwa wakimbizi wa ndani kutokana na zaidi ya nyumba 298,000 kuharibiwa, makazi na kambi. Majengo mengine ya umma pia yameharibiwa, zikiwemo hospitali 453 na shule 1,762. Dhoruba hiyo kubwa pia iliathiri mazingira ya kilimo na rasilimali za maisha, ikiwa ni pamoja na vifaa vya uvuvi.

[Picha: ADRA]
[Picha: ADRA]

"Kimbunga Mocha kilikuwa mojawapo ya dhoruba zenye nguvu zaidi katika miaka iliyopita kupiga eneo hilo. Maelfu ya watu wamepoteza kila kitu, kama vile nyumba, mali, na mifugo yao. Kanisa la Waadventista na mashirika mengine yakuaminika wamekuwa wakifanya kazi kwa karibu na ofisi za ADRA nchini Myanmar na Bangladesh ili kutoa misaada ya kina na kutambua mahitaji ya watu wote walioathiriwa, "anasema Prabhook Bandratilleke, mratibu wa dharura wa kanda hiyo wa ADRA. “Kupitia juhudi zetu za kukabiliana na maafa, tunatoa misaada ya kiuchumi na bidhaa zisizo za chakula, pamoja na kusaidia ukarabati wa nyumba kadri inavyohitajika. Tafadhali waweke watu wa Bangladesh na Myanmar katika maombi yenu huku juhudi za kurejesha hali ya afya zikiendelea. ADRA imejitolea kusaidia jamii kurejea hali yao ya kawaida haraka iwezekanavyo.”

ADRA imekuwa ikihudumia jamii nchini Myanmar na Bangladesh kwa zaidi ya miaka 30 kupitia juhudi za misaada ya kibinadamu na miradi ya maendeleo inayosaidia familia, watoto na wakaazi mmoja mmoja.

The original version of this story was posted on the ADRA website.