South Pacific Division

Washiriki wa Kanisa la Waadventista Wahimizwa Kuchangia Biblia Zao za Ziada kwa Waumini Wapya wa nchini Papua New Guinea

Kampeni ya hivi karibuni ya uinjilisti ya PNG fo Christ ilisababisha idadi kubwa zaidi ya ubatizo katika historia ya Pasifiki Kusini.

Dkt. Nick Kross akiwa na familia moja katika Kijiji cha Konos, wakisherehekea ubatizo kando ya mto.

Dkt. Nick Kross akiwa na familia moja katika Kijiji cha Konos, wakisherehekea ubatizo kando ya mto.

[Picha: Adventist Record]

Divisheni ya Pasifiki Kusini (SPD) inatoa wito wa michango ya Biblia ili kusaidia idadi inayoongezeka ya waumini wapya nchini Papua New Guinea kufuatia kampeni ya hivi karibuni ya PNG for Christ. Kampeni hii ya kitaifa ya uinjilisti ilisababisha idadi kubwa zaidi ya ubatizo katika historia ya Pasifiki Kusini.

“Kuna mahitaji ya dharura na ya kuendelea ya Biblia zaidi,” alisema kiongozi wa SPD Dkt. Nick Kross, ambaye amekuwa akipokea maombi ya mara kwa mara ya kutuma Biblia katika maeneo mbalimbali ya PNG.

undefined

undefined

undefined

undefined

undefined

undefined

undefined

undefined

Huku Biblia mpya za World Changer zinaendelea kupeanwa, idadi kubwa ya washiriki wapya bado wanahitaji kupata Biblia.

Michango ya Biblia mpya au zilizotumika inatumwa kwenye ofisi ya SPD iliyopo Wahroonga, New South Wales, Australia. “Ikiwa wewe au mtu unayemjua ana Biblia za ziada ambazo ungependa kuchangia, tafadhali ziache kwenye ofisi ya SPD. Biblia hizi zitapelekwa moja kwa moja kwa waumini wapya huko Papua New Guinea,” Kross alisema.

Makala asili ilichapishwa kwenye tovuti ya habari ya Divisheni ya Pasifiki Kusini, Adventist Record.

Subscribe for our weekly newsletter