Inter-American Division

Akina Mama Waadventista Nchini Guatemala Wajitolea Kuleta Mabadiliko Katika Jumuiya Zao

Tukio ambalo ni la ajabu lilisherehekea jukumu muhimu ambalo akina mama wamejitwika ili kueneza Injili katika nyanja zao zote za ushawishi.

Kundi la Akina Mama wa Kiadventista waliovalia mavazi yao ya asili kutoka Concepción Chuiquirichapa huko Quezaltenango, Guatemala, wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa kongamano kubwa zaidi la huduma za akina mama lililoandaliwa na Unioni ya Guatemala, Septemba 30, 2023. Zaidi ya akina mama 5,000 walisafiri kutoka pande zote kutoka kote Guatemala na wengine kutoka Mexico, Honduras, El Salvador, na Belize, kukutana kwa ajili ya tukio la siku moja katika Kituo cha Mijadala cha Majadas Zona 11 katika Jiji la Guatemala. [Picha: Unioni ya Guatemala]

Kundi la Akina Mama wa Kiadventista waliovalia mavazi yao ya asili kutoka Concepción Chuiquirichapa huko Quezaltenango, Guatemala, wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa kongamano kubwa zaidi la huduma za akina mama lililoandaliwa na Unioni ya Guatemala, Septemba 30, 2023. Zaidi ya akina mama 5,000 walisafiri kutoka pande zote kutoka kote Guatemala na wengine kutoka Mexico, Honduras, El Salvador, na Belize, kukutana kwa ajili ya tukio la siku moja katika Kituo cha Mijadala cha Majadas Zona 11 katika Jiji la Guatemala. [Picha: Unioni ya Guatemala]

Walikuja kwa wingi wa mabasi kutoka kotekote Guatemala na hata nchi jirani za Mexico, Honduras, El Salvador, na Belize. Zaidi ya akina mama 5,000 waliacha nyumba na familia zao na kukusanyika katika Jiji la Guatemala ili kushiriki katika Kongamano la Huduma za Akina Mama la kitaifa ili kusikia Neno la Mungu, kuomba, kuungana, kujifunza kutoka kwa wenzao, na kushiriki jinsi wamekuwa wakifanya mabadiliko katika jumuiya zao. Tukio hili la ajabu lilitokea katika Kituo cha Mijadala cha Majadas Zona 11 mnamo Septemba 30, 2023.

Kongamano la Kihistoria la Huduma za Akina Mama

"Hili limekuwa tukio la kihistoria ambalo halijawahi kuonekana katika Unioni yetu ya Guatemala," Leticia de Hernández, mkurugenzi wa Huduma za Akina Mama wa Unioni ya Guatemala alisema. Kongamano hilo lilichukua nafasi ya lile la awali mwaka 2016, lililohudhuriwa na akina mama 3,000, aliongeza. “Tuna jeshi kubwa la akina mama wanaowekeza kikamilifu katika juhudi za uinjilisti za makanisa ya mitaa na kufanya kazi pamoja kama wazee wakuu, viongozi wa vikundi vidogo, wainjilisti walei, na mengine mengi, kuathiri ujirani wao kwa karama na talanta ambazo Mungu amewajalia. .”

Kongamano la Huduma za Akina Mama lilitafuta kumsifu Mungu kwa juhudi za uinjilisti za akina mama, huku zaidi ya 3,000 wakijiunga na kanisa kwa wastani kila mwaka kutoka kwa huduma yao, na kuwatia moyo kusonga mbele katika kuwatayarisha wengine kwa ajili ya kurudi kwa Yesu, alisema Hernández.

Kundi kubwa la akina mama walioshiriki katika kongamano hilo ni sehemu tu ya wanawake hai zaidi ya 125,000 katika kanisa lote la Guatemala, Hernández alisema.

Claudia Ruiz Casasola, Waziri wa Imani na Elimu wa Guatemala, na Edna Portales, makamu wake wa waziri, walisifu kazi ya maelfu ya akina mama wa Kiadventista nchini Guatemala kwa kuathiri maisha ya wananchi wengi katika jumuiya zao.

Kutimiza Dhamira

Heather Small, mkurugenzi wa Huduma za Akina Mama katika Konferensi Kuu, aliwahimiza akina mama kuleta mabadiliko ya kweli ambapo wanaweza kuwa na ushawishi mkubwa katika familia zao na maeneo ya kazi. "Ikiwa tutakuwa akin amama tofauti na wengine, ni lazima tumruhusu Bwana ahuishe mioyo yetu - acha Yeye atutie nguvu upya, atufanye upya, aturudishe na atubadilishe," alisema Small. "Lazima tuhisi hitaji letu la Mungu, kuwa na imani, na kukua."

Kila mtu ana matatizo na changamoto, Small alisema, "lakini licha ya hayo, Mungu anatuagiza kwenda kutimiza utume." Aliwakumbusha maelfu ya akina mama kwamba Mungu anaona kila mmoja wao kuwa mtu-mmoja, anajua magumu na huzuni, lakini anampenda kila mmoja wao. "Popote tunapoenda, lazima tushiriki upendo wa Yesu ili watu waweze kuona upendo Wake ukionyeshwa ndani yetu na matendo yetu."

Edith Ruiz, mkurugenzi wa Huduma za Akina Mama katika Divisheni ya Kati ya Amerika na Viunga vyake yaani Inter-American Division (IAD), alihimiza mkusanyiko kukabiliana na hisia zozote za kutotosheleza ambazo zinaweza kuwazuia kukua katika upendo na kukubalika katika Bwana. "Lazima tujione jinsi Mungu anavyotuona na sio kufuata viwango vya ulimwengu vya uzuri, thamani, au kukubalika," alisema Ruiz. "Kamwe usidharau nguvu ya kutumia wakati peke yako na Mungu kwa sababu hakika itabadilisha maisha yako na kukubadilisha na kukusaidia kuleta mabadiliko hapo ulipo."

Kugeuzwa Katika Yesu

Ruiz alikumbusha kundi kubwa la wanawake kwamba wanaweza kuleta mabadiliko makubwa katika misheni mahali walipo. "Sio lazima kuwa na cheo cha kitaaluma, wala haja ya kuzungumza lugha nyingi, wala kuishi katika jiji ili kuleta mabadiliko," Ruiz alisema. "Unaweza kuleta mabadiliko kwa matendo yako, kupitia maisha yaliyobadilishwa ndani ya Yesu kila siku."

Akina mama kutoka kila moja ya konferensi nane walichukua muda kuripoti shughuli mbalimbali za uinjilisti na mipango ambayo wamekuwa wakifuatilia mwaka huu katika jumuiya zao.

"Ilipendeza sana kuona wanawake wengi wakivalia mavazi yao ya rangi wakishiriki katika lahaja zao jinsi wanavyotimiza misheni ya kanisa," Ruiz alisema. “Misheni haijatengwa tu na kundi moja fulani kama wanaume, au wanawake, au vijana, au watoto; ni yetu sote kutumika kama chombo ambacho Mungu anaweza kutumia kutimiza makusudi yake.” Umoja na uungwaji mkono aliokuwa nao kila mama kwa mwenzake ulikuwa wa kuvutia kuona, aliongeza.

Kuokoa Utume

Akina mama wanafuata lengo la Huduma za Kina Mama wa IAD mwaka huu, ambalo linaangazia haja ya kushirikishwa katika utumewa uokoaji. "Akina mama wanaokomboa au kurudisha utume, kuokoa maisha kupitia uinjilisti, kuokoa jamii kwa mipango ya uenezi, kuokoa familia, na zaidi, wakifanya kazi kutoka moyoni kuleta mabadiliko hayo kwa Yesu," Ruiz alisema. “Kusikiliza jinsi ambavyo wamekuwa wakitumia mafunzo ya Biblia, ambayo yametayarishwa mahususi ili wayatumie, na kuona jinsi yameyapatanisha katika mipango na shughuli zao kote Guatemala imekuwa baraka kuona hapa.”

Kongamano hilo lilikuwa sehemu ya mpango mkubwa zaidi ulioongozwa na Kanisa la Waadventista nchini Guatemala kuwashirikisha waumini wake katika kushiriki kikamilifu katika kushiriki Injili na programu za ufuasi ili kuimarisha makanisa na jumuiya zao, alisema Mchungaji Gustavo Menéndez, mkurugenzi wa Huduma za Kibinafsi wa Unioni ya Guatemala. "Maelfu ya akina mama katika makanisa na mikusanyiko yetu wanachangia kikamilifu katika kukuza kanisa nchini Guatemala," Menéndez alisema. Takriban asilimia 30 ya zaidi ya ubatizo 9,000 unaofanyika kote katika unioni kila mwaka ni matokeo ya moja kwa moja ya juhudi za kujitolea za akina mama wanaojishughulisha na mipango ya utume.

Unioni ya Guatemala ina Waadventista Wasabato zaidi ya 195,900 wanaoabudu katika makanisa na mikutano 1,370 katika taifa hilo. Kanisa linaendesha konferensi 5 na misheni 3, shule 30 za msingi na sekondari, pamoja na vituo 2 vya redio ambavyo vinashughulikia asilimia 80 ya nchi.

Gustavo Menendez contributed to this report.

Topics

Subscribe for our weekly newsletter